Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Bei za vyakula zikipanda kama nyakati hizi maskini ndio wanaoteseka zaidi,inabidi wabadili ratiba za milo na kiasi . Ugali ukibaki hautupwi, unaliwa asubuhi na chai.
Maskini ndio wanaoteseka na huduma mbovu za Afya, wanasongamana hospitali, wanachelewa kupata huduma au wanaweza wasipate huduma kabisa.
Kwenye dharura na majanga wao ndio wahanga wakubwa na wanaotaseka zaidi. Mfano katika eneo lenye mafuriko kila msimu bado utawakuta hapo hadi waondolewe kwa nguvu.
Masikini wanaishi kwenye makazi duni, slums ni makazi ya masikini. Unaweza kukuta familia ya watu Watano yenye wanaume na wanawake wanaishi kwenye vyumba viwili vilivyo karibu kabisa na mtaro wa maji machafu
Masikini wanakuwa katika hali ya kukosa usalama zaidi. Ukisikia panya road, tatu mzuka n.k wahanga wake wengi ni masikini.
Kwenye usafiri wa umma wanasongamana na kuvijiana majasho huku pia wanakooleana .
Haya ni machache tu.