Kwangu mimi Messi ni mwamba halisi wa soka kuwahi kutokea duniani. Yaani kadri anapokutana na changamoto mpya na kubwa ndivyo anavyozidi kutafuta kung'aa zaidi.
Nimefuatilia mechi zake huko France nikagundua Messi anaweza kucheza popote na akang'aaa.
Toka ameingia PSG japokuwa ana magoli machache, lakini amekuwa kinara wa assist za magoli, kuisukuma timu kupata ushindi kwenye nyakati zote ngumu. Huyu ni mchezaji ambaye kila kocha angetamani kuwa naye kwenye timu.
Wale wanaompima mchezaji kwa wingi wa magoli, basi kwa Messi wajipe muda zaidi, watakuja kuogopa kulisema tena hili kwa Messi siku chache zijazo.
Binafsi ninaona PSG ikitwaa tena ubingwa wa France na huenda ikabeba klabu bingwa msimu huu kwa msaada wa Messi. Katika hili muda ndio utakuja kunihukumu.