Kwa wale mnao enda kusomea UALIMU,someni hapa.

Chinga One

JF-Expert Member
Joined
May 7, 2013
Posts
11,469
Reaction score
12,391
Habari,
Naam,ndugu zangu mnaoenda kusomea ualimu jueni ya kua nyie ni watu muhimu kwa taifa hili kwa kua in the near future ndio mtakao kuja ku impart knowledge and skills kwa watoto wa kitanzania kama tunavyo fanya sisi walimu tulio watangulia.

Usifurahie tu kwa sasa kupata post ya chuo yakupasa utambue ukisha maliza masomo utapata ajira kwa urahisi sana ya ualimu,kila kazi ina changamoto zake,lakini changamoto za ualimu ni nyingi na zinakatisha tamaa kama hauna uvumilivu waweza ishia njiani,mishahara midogo sana,mazingira magumu ya kufanyia kazi,umbali wa makazi ya walimu na shule,uhaba wa huduma za kijamii huku vijijini mfn umeme,maji,afya,networks,banks n.k, kama una ndoto za kuishi maisha ya kifahari futa kabisa hiyo mentality, ualimu ni full of stress and frustrations kwa wote wa mjini na vijijini.serikali haijari kabisa na haina mpango wa kuboresha maisha ya mwalimu.

Ni bora ukatafakari mara mbili mbili kabla ya kwenda kuanza masomo.sisi kaka/dada zenu tunahisi kama tulipotea njia.

Chinga 1.
 
Serikali hadi leo bado inamuundermine tu mwalimu sasa kwa ujumbe kama huu toka kwa watu ambao wako tayari katika maisha ya ualimu, Je ambao walikuwa na wazo la kuja kuwa walimu ukiwafikia ujumbe kama huu unafikili itakuwaje? Sidhani tunapoelekea kama hii fani itapata watu kabisa, Ila lawama zote ni kwa serikali ambayo ndo ina wajibu wakuhakikisha maisha ya mwalimu yanabadilika angalau kutoka sehemu moja kuelekea nyingine kwa maana sehemu duni hadi inayoridhisha ukiringanisha na hali ilivyo sasa, THINK TWICE.
 
Kozi za ukweli ,zenye heshima ni 5 tu ambazo ni 1.engineering 2.medicine 3.law 4.architecture 5.accounting&finance
 
Umetoa ushauri na changamoto nzuri kwa vijana wetu.
 
hehe umewakata maini vijana wote wanaoenda kusoma ualimu mwaka huu...vijana wanaenda chuo wakiwa na frustrations kutokana na ujumbe wako...
 
Huu ni ukwel mtupu...wenye macho tazameni!!
 
Kwa sababu kozi yako haipo

Dogo siwezi kupoteza mda kubishana na wewe coz nilisha pita level yako since 2006 so ask your self where were u in 2006? kwa hesabu ya haraka utakua umemaliza fm 6 this year then 2010 we ulikua fm 4 ambapo kwa mwaka huo mi nilisha watoa vijana kibao kwenda fm5,kma 2010 ulikua fm 4,basi 2006 you were std 7. endelea kuamini kama unavyo amini.
 
hehe umewakata maini vijana wote wanaoenda kusoma ualimu mwaka huu...vijana wanaenda chuo wakiwa na frustrations kutokana na ujumbe wako...

Kijana sina nia ya kuwakatisha tamaa au kuwatishia but nawapa fact ya mambo jinsi yalivyo ili kama kufanya uamuzi wafanye mapema kabisa isije baadae wakaanza kuleta thread za kuomba ushauri kutaka kuachana na ualimu wakati they have chances to decide now.
 

wamesha chaguliwa huko mkuu...ungewashauri jinsi yakujitoa
 

Mkuu kumbe we mwalimu wa sekondari??
 
dogo mwenyewe amefanyiwa standardization za tokeo lao la necta lakini hajapata matokeo mazuri,so usiwe na dharau kama hiyo,nahisi ukikua utaacha mambo haya ya kitoto
 

Hayo ni mawazo mgando,kama msomi huwezi kwepa changamoto,tumia elimu ulonayo kuzishinda.Nyie ndo walimu fake mnaotegemea mwisho wa mwezi
 
Hayo ni mawazo mgando,kama msomi huwezi kwepa changamoto,tumia elimu ulonayo kuzishinda.Nyie ndo walimu fake mnaotegemea mwisho wa mwezi

Sawa mdogo wangu ndo maana nakupenda sana umenena ukweli mtupu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…