Kwa wale mnaoanza biashara zingatia haya

Kwa wale mnaoanza biashara zingatia haya

TheForgotten Genious

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Posts
2,087
Reaction score
3,156
Kijana kama unataka kuanza biashara ili uweze kufika pale unataka hakikisha mambo haya una yazingatia

1.Panga chumba ama jengo la biashara kwa mtu ambaye ni muelwa hii itakusaidia kipindi ukikwama kodi.

2.Kuwa muwazi kwa baadhi ya mambo kwa mmiliki wako wa jengo hili litakusaidia kukuvumilia .

3.Kama umechukua mkopo hakikisha biashara uliyoichukulia mkopo ndio inafanya rejesho.

4.Jenga uhusiano mzuri na maafisa mikopo hii itakusaidia kukupunguzia pressure kipindi unapokwama kufanya rejesho.

5.Kamwe usijenge hofu dhidi ya wadai wako na wala usijenge mazoea yakuwadanganya pindi unapokwama.

6.Toa taarifa mapema endapo utashindwa kufanya rejesho.

7.usifanye maamuzi kwa haraka kwa sababu ya changamoto.
 
Mjinga ndio uanzisha biashara kwa pesa ya mkopo aliyopewa na maafisa
 
Back
Top Bottom