Kwa wale mnaopenda kula hotel ya Aljazeera

Al jazeera hotel ilikua zamani sio sasa.bora ule comfort
 
barabara ya dodoma iringa kupitia mtera ndio balaa,,hizo hotel mabasi yanaposimama kula ndio utachoka kabla hata haujashuka kwenye basi
 
Hapo aljazeera nshakula sana mishikaki katika safari zangu za kwenda Iringa.

Kama nilikula nyama ya mbwa potelea mbali.

Nachojua mishikaki ilikuwa mitamu na nilikuwa na njaa.

Heck, ignorance is bliss.
 
Pale hamna kitu, msosi bei kubwa halafu haueleweki. Wali na ugali huwezi kutofautisha.

Mimi sababu mara nyingi basi ninalopanda huwa linakula pale, basi nimejigundulia mama nitilie yupo pale pembeni yake wali nyama 2000 Safi kabisa.
 

Mkuu umenena. Kiukweli, hiyo ndo route pekee yenye sehemu za maana za kula. Nenda hata route ya Mwanza, tokea popote, ni majanga.
 
Comfort napo chenga kabisa hakuna lolote kwenye hii njia huduma za vyakula ipo chini sana bora kula nyama choma kwa Masai
 
Umeniwahi Liverpool ni kama Aljazeera afadhali ule gengeni kuliko hapo,hawa waarabu tamaa zimewazidi uchafu wao wanauleta hadi kwenye biashara

Pamoja na ubaya wa L'pool, mtori wao mtamu sana. Anaouza yule mama.

Btw, ukipanda Hood lazima ule pale.
 
Si hapo2 ni sehemu kibao,,,,,,yaan huduma ni mbovu isana
 
yan iyo hotel siipendi hata kuisikia kwanza chakula bei ipo juu alafu vyakula vyenyewe ni viporo
 

Liverpool ile ya Mombo au nyingine? Kama ni ile ya Mombo endelea kula UCHAFU.
 

ukipita highway pale kuna nyama choma ya mbuzi ime andaliwa kwa uzuuri kabisa.....huko iringa road hakuna cha aljazeera wala confort kote chenga tu.
 

mi nikifika aljazeera zaidi ya kwenda toilet na kununua juice take away hakuna cha zaidi pale.
 
safarini usile wali, ugali, ndizi.

Kula dried foods. Karanga, biscuits. Na maji lako la kilimanjaro mpaka home.
 
niliwahi safiri na mdada mmoja yaan yeye samaki kanunua kala.. mahindi ya kupika kala... yai ka kuchemsha kala.. juice zetu zile ndo anakunywa tuu.. kufika sehem tena ananunua hizo chips.. nikawaza hivi huyu tumbo likimvuluga sasa hivi hapa si ndo itakuwa mwisho wa safar huyu.....
kiufupi si vizur kulakula njiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…