Kwa wale PHP developers angalia hii video kisha endelea na kazi zako

Kwa wale PHP developers angalia hii video kisha endelea na kazi zako

Siku hizi nasikia wengine wanaisifia Python na kuiponda PHP. Shida nini?
 
Siku hizi nasikia wengine wanaisifia Python na kuiponda PHP. Shida nini?
Kulinganisha au kushindanisha PHP na Python kwenye kazi moja ni makosa.
Python ni bora sana kwenye mambo fulani na PHP inarahishisha kazi au tuite bora kwenye mambo mengine.

Python ni lugha ya wanasayansi hasa mathematician, huko ipo bora kuliko PHP.

Huu ni mtazamo binafsi.
 
Sijui kwanini siku hizi nikianza kuangalia video za programming nasinzia fasta.
 
Sijui kwanini siku hizi nikianza kuangalia video za programming nasinzia fasta.
You're not serious bro, kuwa na muda wa kupumzika na pangilia namna unavyosoma kwamba unaanzia wapi kwenda wapi na muda upi utamaliza unavyosoma.

Kuna aina mbili za kusoma programming lakini kabla ya yote uwe na research ya kipi utasoma na kwanini.

1.up and running- Hii inachosha ukiwa mzembe kusoma huku unafanya, kwa mtu asiye na uzoefu atleast two pl ni ngumu kuitumia hii njia, mara nyingi inapendeza ukiwa na computer mbili.
2.Read, note and practice.
Hii inaeleweka zaidi ijaribu, hii ukiwa na hardcopy books ni nzuri sana ila si lazima maana softcopy zinachosha macho sana .

Mimi hutumia vitabu na pamplets za programming nimetumia njia hii na niko vizuri.

Hii up and running natumia mara chache sana.

Jaribu kuwa na ratiba nzuri usingizi utausahau
 
Back
Top Bottom