Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mzee ulikua unakaa na mzazi mmoja eh?WanaJf habari za Leo unajua enzi utoto wengi tumepitia katika maisha tofauti tofauti ebu wale tulikuwa wadokozi tukumbushane hapa unakumbuka nini na uliwahi kukamatwa na kupewa adhabu?
Ipo hivi kwetu baba baada ya kustaafu shirika la reli (marine) alirudi nyumbani na kuwa mfugaji, nakumbuka nilikua mpenzi sana wa maziwa mgando (hadi leo) sasa maziwa yetu (watoto) baada ya kuchemshwa yaligandishwa yenyewe na ya baba yenyewe kwenye kibuyu flani hivi kwenye nyumba ya mamdogo mzee alikua na wake watatu.
Siku moja nilitoka shule nikiwa na njaa kinoma siku hiyo sikurudi lunch make shule ilikua mbali ilipogongwa kengele ya sa tisa nikatoroka kuwahi kiporo changu nkakuta wenzangu hawakunibakishia moja kwa moja hadi kwenye kibuyu chetu napo hola.
Nikatimba nyumba ya ma mdogo kuingia Jikoni nikapekua chungu nikakuta samaki sato hilo nikajipakulia katikati mkononi nikaenda kukaa mbali kidogo nikamaliza.
Kuangaza huku na huku ni watoto wadogo tu ndo wanacheza hawana habari na Mimi nikarudi ndani nikamalizia lenta hawamu hii sikuacha hata kichwa nikaenda kulekule nikafyekelea mifupa nikawapelekea mbwa.
Kuangaza huku na huku bado watu hawajarudi ikawa zamu ya maziwa ya baba kwa bahati mbaya yalikua yanawekuwa juu ya kabati la vyombo jikoni na Mimi sifiki nikachukua stuli lilikua limelegea misumari kwichikwichi nikalisogeza nikapanda kuchomoa kibuyu ile naliweka begani sijui mguu ulifanyaje nikasikia kwich nikajua ndo nimelimalizia stuli ule uoga maziwa yalikua mengi kwenye kibuyu nayo yakaanza kutikisika, sijakaa sawa nikajikuta Niko chini kibuyu kimepasuka na maziwa yameniosha mwili mzima.
Heeee!! Nilinyanyuka akili ya kwanza ikanambia nikawafungulie mbwa waje wayalambe Yale maziwa pale sakafuni nikakimbia kwenda kuwafungulia nilipowafikia kwanza nilichuchumaa ili waanze na Mimi wakanilamba moja akanilamba mdomo nikanyanyuka sikuwafungua nkasema hapa nitakutwa na watu wakirudi watanikuta na wakinikuta itakuwa soo na nitapigwa na mama wote alafu mzee atakuja fanya finishing ya nusu kifo.
Nilikimbia nikachukua begi la shule na sare huyoo mpaka mtoni kupitia vichakani nikavua nikaoga nikafua bila sabuni nikaanika hukohuko kichakani nikavaa sare nikakaa huko kichakan nikahakikisha wote wamerudi ndo nikajitokeza, siku hiyo watu walipigwa Mimi tu ndo sikupigwa kwa sababu nilichelewa kurudi nyumbani.
Na niliwakuta akina mama wote wapo, msione haya maelezo ni marefu lakini hii action haikuchukua hata dakika kumi.
Umenichekesha sana mkuu. Akili ilitumikaIpo hivi kwetu baba baada ya kustaafu shirika la reli (marine) alirudi nyumbani na kuwa mfugaji, nakumbuka nilikua mpenzi sana wa maziwa mgando (hadi leo) sasa maziwa yetu (watoto) baada ya kuchemshwa yaligandishwa yenyewe na ya baba yenyewe kwenye kibuyu flani hivi kwenye nyumba ya mamdogo mzee alikua na wake watatu.