SoC02 Kwa wale waliokata tamaa

SoC02 Kwa wale waliokata tamaa

Stories of Change - 2022 Competition

Amani Dimile

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
243
Reaction score
399
KWA WOTE WALIOKATA TAMAA KWENYE MAISHA YAO 🙏🏽

Kwa wote waliokata tamaa juu ya maisha yao, kwa wote ambao tumaini lao limeshapepea mioyoni mwao. Kwa wote waliojawa na wasi wasi na katu hawana imani thabiti kabisa. Someni hii, huenda ikawasaidia 🤝🏼

Ujumbe huu upo kwa ajili ya kukumbusha kuwa, huwezi kuwa kila kitu kwa kila mtu na kwa kila siku. Yaani utajitahidi sana kuwa wa maana kwenye maisha ya watu lakini wapo ambao watakupuuza. Lakini pia wengine watakufanya wa maana lakini si kwa muda wote. Binadamu wamejawa uongo, unafki na kukinai.

Ndani ya muda wowote unaweza kufanyiwa jambo lolote, na mtu yeyote bila sababu yoyote. Usiwaze, usilie, wala usiumie jipe moyo, asubuhi mpya ya tumaini ipo njiani karibuni itapambazuka.

Kaa chini, zikumbuke zile siku za zamani ulizokuwa ukicheka, zile siku ulizokuwa na furaha. Siku zile ambazo ulikuwa na amani tele sababu kila jema lenye kheri lilikunyookea.

Kumbuka unatakiwa ujisamehe wewe mwenyewe mara kwa mara maana wewe si mkamilifu, una mapungufu na u kiumbe dhaifu.

Jikumbushe kuwa huwezi kulazimisha kila kitu kiende kama unavyotaka, ndio huwezi nasema tena huwezi kulazimisha kila kitu kiende kama unavyotaka. Kuna muda inabidi usimamie ukweli wa moyo wako hata kama unauma kiasi gani. Jifunze sana kulinda hisia za moyo wako, kuna muda jibu la HAPANA ni la muhimu sana na litalinda amani ya moyo wako kuliko kujibu NDIO kisa tu una shida ya furaha ya muda mfupi (Itakugharimu mpenzi).

Usikae ujutie wale watu ambao wameondoka kwenye maisha yako hata kama uliwahitaji kiasi gani, kumbuka stori ya maisha yao kwenye kitabu chako cha maisha imeisha hivyo huwezi kulazimisha waendelee, huwezi ndio huwezi.

Fahamu ya kuwa wewe una kasoro zako, hivyo wapende sana watu ambao wanakupenda na kukujali vivyo hivyo na kasoro zako. Yote kwa yote jiamini, muamini yule aliyekuumba kamwe hawezi kukuacha mpweke uamini pia na ujumbe huu utaponesha maisha yako.

Hivyo kama ulianza kukata tamaa, huu ndio muda wa kuamka tena. Futa machozi, tabasamu sema kimoyo moyo 'asubuhi nyingine ya furaha i njiani inakuja'. Yes inakuja, ndio inakuja niamin mimi inakuja 😁

Mungu akujaaalie maisha mema yenye furaha tele 🤲🏽

Wako katika kalamu Amani Dimile
 

Attachments

  • WipeOut20_26_2022_082026.962000.jpg
    WipeOut20_26_2022_082026.962000.jpg
    27.5 KB · Views: 9
Upvote 0
Back
Top Bottom