Kwa wale waliowahi kupewa adhabu bila sababu za msingi

Kwa wale waliowahi kupewa adhabu bila sababu za msingi

Nyambiza jr

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2018
Posts
1,033
Reaction score
1,841
Kuna adhabu nyingine unaipata unashindwa kujua kabisa kwanini nimepewa adhabu hii hasa kipindi cha utoto kuna adhabu za kionevu sana. Mimi za kwangu ni hizi kila nikizikumbuka naonaga ni uonevu tu :-

1. Kuna siku nimechelewa Madrasa kwa sisi tuliokulia ktk dini ya kiislaam baada ya kurudi shule saa 8 inabidi ule halafu uelekee Madrasa, sasa siku hiyo home chakula kilichelewa ikabidi nisubiri chakula kwanza mpaka nakuja kumaliza kula ikawa imefikia kama saa 10 na nusu baada ya kumaliza kula ikabidi fasta nijiandae niendee Madrasa kufika huko Ustaadh ananiuliza kwanini umechelewa nikamwambia sababu daah unaambiwa alinilaza chini na kunipiga stick za kufa mtu akaniambia nakuadhibu kesho uwaambie wakupikie mapema.

2. Nyingine niko home nakunywa chai na vitumbua baada ya chai kuisha kwenye kikombe nikaona bora kitumbua changu kilichobaki nikalie nje maana kulikuwa na michezo wenzangu walikuwa wanaendelea kucheza nikaona km nachelewa. Basi ile kutoka nje na kitumbua bi mkubwa aka mind akaniita ndani kwanini umetoka na kitumbua nje kalete fimbo basi daah nikachezea stick

3. Jingine ninalolikumbuka, kitaa kulikuwa na mechi ya mpira wa miguu kati ya watoto wa kiume wa kitaa na wakike hii mtaani kwetu huwa bonge la mechi km la watani wa jadi. Basi siku hiyo ili niwahi mechi baada ya kuruhusiwa shule ikabidi nivue viatu niweke kwenye Begi alafu nianze kukimbia maana Mimi nilikuwa nasoma mbali na ninapoishi tofauti na wenzangu wengi walikuwa wanasoma karibu kwa wakazi wa Dar nadhani mnaijua Shule ya msingi Mugabe alafu Mimi nilikuwa nakaa Sinza kwa Remy wenzangu wengi walikuwa wanasoma Mashujaa primary school. Basi nikaanza kukimbia kuwahi game homu na Mimi nilikuwa mchezaji tegemeo kufika home nakuta wenzangu ndio wameshajipanga kwa mtanange Mimi nikachoma home fasta kwenda kuchange nguo niingie uwanjani kuingia ndani nyumbani niko peku navuja jasho kwa kukimbia Dada zangu wacha wanishambulie kwa maneno makali ya kinoko na wakajua sababu ni ile mechi basi bi mkubwa ikabidi anizuie nisitoke nje hadi usiku uingie daah nililia sana siku hiyo nikaona huo ni uonevu wa kupindukia.

Najua humu wengi watakuwa wamepitia maisha km haya kuna zile adhabu za kupiga kelele darasani ticha akija ni stick kwa woote hata waliokaa kimya wakawa wanajisomea inauma sana

Hebu wadau tusimuliane jinsi ulivyopewa adhabu bila sababu za msingi wengine km haijawakuta udogoni unakuta hata humu ukubwani kwa waajiri wao, wapenzi wao nk. ....

TIRIRIKA TUFURAHI
 
Hizo Adhabu ni Nzuri sana, Maana hupima temper na uwezo wa kujicontrol wa Muhusika
 
Mbona maelezo yako yanaonesha sababu zilikuwa za msingi kabisa??
 
niliwahi kumkabidhi demu wangu mimba, mama yake akampa adhabu ya kumfukuza huyo binti na kuja kuishi geto kwangu. hakika nilifurahi adhabu hy.
 
Back
Top Bottom