Hii ni kwa wale wote wenye mapenzi au wanaovutiwa na shughuli za kilimo na ufugaji hususani ufugaji wa samaki
Tuna toa huduma ya kuuza Vifaranga/mbegu bora ya samaki aina ya Sato (Nile Tilapia)
Mbegu zetu ni nzuri Sana kwanza kabisa wana-uniform size, samaki wanakuwa haraka ndani ya muda mfupi, wanastahimili magonjwa na mabadiliko ya ubora wa maji
Bei ni Tsh 200 - 300 kwa kifaranga kimoja, chenye uzito kati ya 1g - 10g
Tunapatikana Mingoi, mbele kidogo ya Bunju B njia ya kuelekea Bagamoyo, pia tuna tuma mzigo kwa wahitaji waliyopo nje ya Dar/Pwani
Ni sahihi nilitamani nianzie huko Ila nikaona andiko litakuwa refu sana na kimsingi andiko hili liliwalenga wale ambao wanauelewa kuhusu ufugaji samaki
NAELEZEA KWA UFUPI
Ufugaji wa samaki unahusisha kuzalisha, kulea na kuwafuga samaki nje ya mazingira yao ya asili
Ufugaji wa samaki unaweza kufanywa kwa njia ya bwawa, tank au hata ziwani kwa njia ya vizimba, muhimu ni kuwa na maji ya kutosha (maji baridi kwa Sato/kambale)
Chakula cha samaki, Kuna chakula cha aina mbili chakula cha asili cha samaki, mimea midogomidogo na wadudu (zooplanktons & phytoplanktons) Hiki uzalishwa baada ya kurutubisha maji kwa kutumia mbolea ya Ng'ombe, kuku n.k
Aina nyingine ya chakula ni chakula cha kutengenezq, Hiki akitofautiani Sana na kile cha kuku ingredients ni kama vile Pumba za mahindi/mpunga, dagaa/uduvi, mashudu ya pamba au alizeti n.k. Pia unaweza kununua chakula ambacho kipo tayari Kuna supplier wengi wanauza chakula kutoka nje ya nchi
Mambo mengine ya kuzingatia, kulisha kutwa Mara 2 hadi 4 kwa samaki wadogo, kuwalisha kulingana na uzito wao kwa wastani samaki anakula 5% ya uzito wake kwa siku, kupima uzito wao (sampling) kila mwezi ili kujua maendeleo ya ukuaji, kubadilisha maji at least mara moja kwa mwezi
Uzuri wa samaki case za magonjwa ni nadra sana, awahitaji chanjo wala madawa katika ukuaji wao, samaki ni watumiaji wazuri wa chakula unachowalisha ukimlisha let's say 1.5kg tarajia kupata samaki mwenye uzito wa 1kg na pia Samaki (Sato) ni kitoeo kizuri kinapendwa na karibu jamii yote ya Tanzania
Vitu ni vingi siwezi kuandika yote nikamaliza Ila kama unavutiwa na ulitamani kujifunza zaidi naweza kukuunga kwenye group letu ukajifunza zaidi