Kwa wale wasiojua umuhimu wa Katiba nzuri

Kwa wale wasiojua umuhimu wa Katiba nzuri

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Bado nashikilia nadharia kuwa ni bora zaidi, hasa kwa nchi isiyo na uwezo mkubwa, kuvifanyia marekebisho vipee vibovu vya Katika (Constitutional ammendment) badala ya kuandika upya Katiba nzima. Nilitoa sababu tano za na hoja za kupendelea zaidi (Constitutional Ammendment).

Leo nataka tu kuonesha kuwa Katiba mpya, au hata ile ya kusawazishwa, ni muhimu sana kwa maendeleo ya kiasa, jamii na hata uchumi. Kuna mwanasiasa alisema Katiba si muhimu, muhimu kwanza ni kutengeneza uchumi. Hilo halikuwa sahihi.

Kenya, ambayo katika miaka ya tisini hadi 2005 haikuwa hata katika 'kumi bora' za Afrika kwa uchumi...ghafla ilipaa na kuwa ya kumi,tisa, nane hadi ya saba kwa uchumi mkubwa Afrika hii leo, mara tu baada ya kubadilisha Katiba yake hapo 2010. Leo hii Nairobi inakumbatia Makao makuu ya kanda ya mashirika kama Coca Cola, Google, IBM n.k. kwa vile wawekezaji wakubwa wana imani na utawala wa sheria uliowekwa na Katiba mpya ya Kenya.

Halkadhalika katika maendeleo ya siasa na jamii. Mtu yetote aliyetembelea Kenya miaka ya '90 ataona maajabu makubwa ya mabadiliko- uhuru wa watu, maeneleo makubwa ya miundo mbinu, internet, habari na pato la mtu wa kawaida.

Isingewezekana kwa vyovyote vile kwa haya kufikiwa bila ya kufanya marekebisho/ kubadilisha katika.

Mwenye kusikia asikie.

Infographic: Africa's Biggest Economies | Statista
 
Back
Top Bottom