Jocasta
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 474
- 595
Mwaka jana mwezi wa nane baba aliniita nyumbani akaniomba nimununulie chupa kwaajili ya kuwekea chai (japo ilikuwepo).
Pia akaniomba kabla ya kuondoka nimununulie redio, alifurahi sana kufanya alichoniagiza.
Sikujua ya kwamba kumbe hivyo vitu viwili nilivyomnunulia ndiyo vya mwisho kabisa kabla ya kutamatisha maisha yake duniani.
Mwezi wa kumi na mbili wakati nikiwa ziara ya kikazi Mbeya, nilipigiwa simu na mama akiwa analia kwa uchungu na akanisihi niende nyumbani haraka sana.
24/12 nikifika nyumbani nikashangaaa kumuona baba yangu akiwa kwenye wakati mgumu sana. Siku iliyofuata aliaga Dunia.
Nililia sana tena sana, hadi mda huuu huwa nalia. Baba wa Mbinguni toa faraja kwa watu wako waliopoteza wapendwa wao.