Kwa waliofiwa na baba zao njooni hapa tufarijiane

Ahsant sana kwa faraja
 
Sina mengi ya kusema zaid ya kumuombea pumziko jema kweny ulimwengu wa kiroho

I miss u pops, nataman sana ungewaona wajukuu zako..
 
Baada ya mzee kufariki nikaea napekuwa nyataka zake ndio nikagundua hakuwa mtu wa kawaida alikuwa na akili nyingi mithili ya robot au komputer
Ila tujitahidi sanaa kua mifano bora kwa watoto wetu.. mtoto atakumbuka daima umahiri wa mzaz wake.
 
Poleni sana, wapendwa,nimelia mnooo,mpaka Sasa nalia sijui ntafanyaje ili niweze kusahau,
Mpaka Sasa naliona hili kwangu nizito,mzigo huu umekuwa mzito Sana kwangu,

Mpaka Sasa natamani kusahau,Ni mwaka Sasa unaelekea kuisha japo nashindwa

Maumivu huwa hayaishi, u learn to live with the painful fact
 
Yani Kuna siku nipo na rfk zangu tunaongea nkaanza kulia wananiuliza una shida gani nkawaambiwa nmemkumbuka baba angu.
Sijawai kupona siwez kusema zaid.
Nakukumbuka sana baba angu
 
Yani Kuna siku nipo na rfk zangu tunaongea nkaanza kulia wananiuliza una shida gani nkawaambiwa nmemkumbuka baba angu.
Sijawai kupona siwez kusema zaid.
Nakukumbuka sana baba angu
Pole Sana
 
Baba yangu ndio niliye mtegemea kwa mawazo yake ya hekima na ufahamu
Mwenye Enzi Mungu alinitumia mimi kama ngao wakati anaumwa, nilikuwa nampeleka hospital za nje pale ambapo naona Tanzania bado hatujapata vifaa muhimu vya tiba!
Hivyo nilikuwa naye kama mtoto wa kiume, mpaka hapo atakapo pata nguvu yote!
Kwa bahati mbaya nilisafiri kwa muda wa miaka takriban mitatu, huku nyuma baba yangu aliugua sana na ndugu zangu ambao ni waroho wa pesa hawa kuahangaika naye mpaka akafariki [emoji24][emoji24][emoji24]
,Masikini baba yangu [emoji24][emoji24]
Siku wananiambia baba yangu amefariki na wako njiani kupeleka mazishi Moshi,[emoji24][emoji24][emoji24] yaani nilichanganyikiwa kabisa kabisa walahi!
Namshukuru sana Mwenye Enzi Mungu kwa kunipa Baba mwema na mwenye upendo mwingi sana katika maisha yangu, na ilikuwa makusudi ya Mungu kuniondoa ili aweze kumchukua mtu wake walahi!
Ninalia kwa uchungu sana baada ya kusoma death certificate yake imeandikwa cause of death ni negligence [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24] ina maanisha ndugu zangu hawakumjali kabisa mpaka akapata umauti walahi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]!
Duh hii mada imefungua kidonda upya, acha tu nilie walahi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mwaka jana wakati nimeenda kumuangalia tuliongea mengi, na siku naondoka alinikumbatia akasema kwakuwa nimekuona mwanangu hapa nitakufa kifo chema [emoji24]
Nililia sana na kweli baada ya wiki mbili napigiwa simu mzee amefariki [emoji24][emoji24]
Upumzike kwa amani baba yangu mpendwa
 
Baba yangu,rafiki yangu,mwenye upendo mwingi,nalukumbuka saaaana,miaka 15 toka utwaliwe,tulikuwa wadogo Sana lkn Cha maana ulichotuzawadia no kuoa mwanamke mpambanaji mwenye akili nyingi saaana,ashukuriwe Mungu nimepata mme anayenithamini na kuwapenda wanangu km ulivyokuwa unanipenda baba angu....tukutane asubuhi njema baba!!!
 
Pole mkuu
 
Miaka 12 sasa tangu nimpoteze baba yangu.

Ninaishi katika yale mema yote aliyonirithisha.

Mungu ampumzishe salama huko Mbinguni.
 
Maisha yana mengi sana ambayo kwa upande wa Maumivu sio tu kuhusu Baba... Mama pia.

Wengi tuna kumbukumbu za kuumiza sana! Mungu Ni Mkuu sana na anajuwa maumivu yetu.

Tuzidi kumuomba na kumshukuru maana tunapita kwenye Mipango yake.
 
Binafsi ni kama nimefiwa na baba wawili.Mwaka 1999 Baba yangu mzazi Alifariki,Nikachukuliwa na Shangazi yangu. Nililelewa na kusimeshwa na mjomba wangu tangu chekechea mpaka chuo kikuu mpaka napata kazi(Mjomba alikuwa Baba)So Mwaka 2021 Alifariki.Now sina mtu wa kumuita Baba toka moyoni.

Pumzikeni kwa Amani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…