kwa waliopita skauti mko wapi?

Lucas

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
2,457
Reaction score
1,110
jamani mie leo nimekumbuka enzi za skauti na chipukizi (zamani kila mwanafunzi ilibidi apitie chipukizi) nimekumbuka zile nyimbo na mazoezi tuliyokuwa tukifanya nimezikumbuka pia hizi

1. akapusipusi.......malizia
2. skauti wiii.........malizia
3...................................... na wewe eendelea

nimekumbuka pia na wimbo huu "maskauti makomandooo lele lele makomandooo" wewe unakumbuka wapi hiyo?
 
Mie hao jamaa nilikuwa siwapendi, kwanza walikuwa waonevu, pili waliwah kuninyang'anya mzura wangu enzi hzo na kunipigisha push-up waliponikamata natoroka skuli saa mbili usiku, basi toka hapo mie na hao jamaa ni chui na paka.
 
Du! mie na kusahau nishaisahau hiyo skauti, tangu mwaka 1986 Mzee Ally Hassan Mwinyi alikuja makao makuu yetu Upanga, akatuvisha beji, Bahada ya kuwa tumeweka kambi kwa wiki nzima kwenye pori la chuo kikuu kipindi hicho.

Yaani siku ya mwisho siwezi kuisahau tumetembea usiku kucha kwa miguu kuanzia chuo kikuu, mwenge, sarender bridge, ocean road, central police, fire, magomeni, manzese, mpaka chuo, kukawa kumeshakucha.
Ilikuwa noma watoto wa mama mbona walitoroka. Du hapo ndio mwanzo wa ukakamavu ilikuwa. Na uwanja wa taifa tulikuwa tunaingia bure, tunakaa pembeni ya uwanja kuokota mipira.
 
Mie hao jamaa nilikuwa siwapendi, kwanza walikuwa waonevu, pili waliwah kuninyang'anya mzura wangu enzi hzo na kunipigisha push-up waliponikamata natoroka skuli saa mbili usiku, basi toka hapo mie na hao jamaa ni chui na paka.

ilikuwa wapi hiyo iringa? ahah ahha hahpole sana
 
sikioni kitufe cha like, ila nimeipenda hiii, ukakamavu, ujasiri, na kutokuogopa hivi vitu hata mimi skauti ilinisaidia sana
 
Nyie ndio mliosoma mjini shule za wajanja?

Wengine skauti tumeishia kuona kwenye TV ukubwani.

ah afadhali hujapitia lol maana ningetengeneza bifu na wewe, hao watu wamenitesa sana enzi zile Jite hahahaha
 
Mie hao jamaa nilikuwa siwapendi, kwanza walikuwa waonevu, pili waliwah kuninyang'anya mzura wangu enzi hzo na kunipigisha push-up waliponikamata natoroka skuli saa mbili usiku, basi toka hapo mie na hao jamaa ni chui na paka.

Kweli mzazi hawa jamaa walikuwa na mikwara sana, na biti zao za kuchemsha maji kwenye mifuko ya plastiki mara wachemshe yai kwa kulifukia chini.
Nilishuhudia dogo alivunjika wakati anatembea kwenye kamba,
Mzee Muhando alitubembeleza sana ila ah wapi niliapa kuwatema hao watu.
 
halafu naona kama umaarufu na heshima ya scout kama imepungua!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…