Ukishakuwa na F hata moja tu, tayari unakuwa huna FTC. Hapo kusonga mbele inakuwa kagota kwakuwa hata cheti chenyewe anakuwa hajapewa.
Mkuu cheti hana, ni result slip toka barazacheti amepataje? ila kwa DIT naona sijui inakuwaje wanapta vyeti maana kunajamaa yangu nilimuona anacheti lakini ana F ya somo moja. kwa vyuo kama MTC (MIST) na Arusha tech. kama hujaclear hupati cheti
Kama kaamua kurudi kwenye kusaka elimu, basi afanye private candidate Form VI.Najua mpaka kwenda DIT ni kwamba alifanya vizuri paper ya F IV.Mimi ndivyo nilivyofanya na nikajoin UDSM.Asikate tamaa,bado future ipo.
Jaribu UDSM kozi kama Bussiness Administration wanakuchukua!!Wana bodi hamjambo?
Kwa wataalam waliopitia level hii ya FTC ninomba kujua kama mdogo wangu anaweza kupata chuo cha kuendelea na elimu juu kwani ana B moja ya mathematic, C tatu, D moja na F moja ya FTC in highway engineering kutoka D.I.T mwaka 2002. Alishindwa kusuppliment kutokana na kupitiliza muda wa miaka 3 ambayo ilikuwa maximum duration ya kusup. Naombeni ushauri wenu, nifanyaje ili aendelee na elimu zaidi. Mods nisameheni kwani najua wengi wanapita jukwaa la siasa. Mbarikiwe sana