Kwa waliosoma shule za msingi Iringa mjini miaka 90

kweli ya kale ni dhahabu natamani kweli enzi ingekuwa inarudi. nakumbuka nilivyokuwa napenda mikusu, misaula, maembe mabichi ya chunvi, kabla ya kuhamia wilolesi nilikuwa Njombe katika shule ya Mpechi primary school, nilikuwa na marafiki zangu , vinga, Roida,sevanu, nawakumbuka sana tangu tumeachana sijawahi kusikia habari zao wala kukutana nao.
 

imenikumbusha shule ya msingi wilolesi tulikuwa tunakula sana mifudu pale shuleni.
 
Kuna yoyote aliyesoma sabasaba kuanzia 1992 - 1998?
 
nimesoma ubungo N.H..nilimaliza mwaka wa 1999..shule yetu ilikuwa vizuri kwa mchakamcha, fujo pia tulikuwa tunaziweza tambaza,makurumra mugabe walituogopa..nakumbuka wamasai walikuwa wanakamata sana wanafunzi watolo na wavuta bangi..wengi tulikuwa vijobu(wategeaji kuingia darasani) sana enzi hizo tunaacha masomo tunaenda mugabe au mlimani chuo kikuu au nyuma ya bonde la perfect vision high school kupoteza mda..tulikuwa wazuri kielimu na kimichezo asa umitashumta na sanaa pale mlimani enzi hizo kulikuwa na matamasha ya mashule kimashindano yalikuwa yanafanyika chuo kikuu cha mlimani tulikuwa tunawakilisha vizuri sana (nakumbuka ule wimbo wa tamasha tamasha 98 tamasha tunaimba imba tamasha tunacheza cheza tamasha kalibuni nyote" nawakumbuka wakina shira..saidi..mwalabu jimmy..na mwalimu mmoja wa kiume wa somo la kiingeleza hivi alikuwa anapiga bakora hatari..mie nilikuwa naudhuria kipindi cha dini tu sababu kulikuwa kuna mwalimu wa hadithi alikuwa anatuadithia hadithi nzuri na mawaidha nilikuwa nampenda ila jina nimelitoka..kifupi nilisota sana shule ya msingi ila kwa sasa nipo vizuri na chuo ninemaliza...nikikumbukaga mambo ya shule ya msingi machozi yananitoka..walio maliza UBUNGO N.H MWAKA WA 1999..TUKUMBUKANE
FADHIL..
 
Hivi zamani kulikuwa kuna umuhimu wa tuisheni kweli?
 
Luvinga aliyekuwa mkufunzi Wa kleruu college
 
Nilianzia shule pale Makanyagio, nikahia nyumbatatu, then sabasaba tangu la pili mpaka namaliza. Wale waliomaliza 1995 sabasaba tutakuwa tunafahamiana vizuri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…