Kwa Wamiliki wa Band na wanamuziki wa Dansi wekeni kazi zenu mtandaoni

Kwa Wamiliki wa Band na wanamuziki wa Dansi wekeni kazi zenu mtandaoni

Amaizing Mimi

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2019
Posts
489
Reaction score
1,102
Salamu kwenu wabamuziki na wamiliki wa bendi za muziki wa dansi.

Kwanza niwape hongera kwa kazi nzuri ya kuburudisha, kuelimisha na kuhabarisha jamii.

Pamoja na kuwa mlifanya kazi nzuri sana muska hiyo, changamoto tunayopata sisi wadau wenu ni upatijanaji wa kazi zenu mtandaoni.

Leo hii ukitafuta wimbo wowote wa Mbaraka Mwinshehe au Marijani Rajabu ni rahisi kuupata kuliko kutafuta wimbo wa dansi kuanzia 2000's.

Mnashindwa wapi kuweka kazi zenu mtandaoni wadau tuburudike?

Pongezi kwa Twanga pepeta walau nyimbo zao nyingi zinspatikana, bendi kama TOT band ni nyimbo chache sana zinazopatikana.

Stono musica utakuta kuna nyimbo tatu au mbili tu.

Band zifuatazo ndio kabisaa!
Nina Musica, Mviko sound, Mokibo sound, siwezi kutaja zote lakini ukweli ni kwamba kuna mahali mnatukosesha burudani.
Mnashindwa na waimba matusi na amapiano?

Hebu fanyeni namna wekeni kazi zenu mtandaoni.

Naomba kuwasilisha
 
yaani uupate wimbo wa mbaraka mwinshehe then utake wimbo wa dansi wa 2000 ukose?? sio kweli.

we ulitaka wimbo gani ukaukosa?
 
Wataziweka soon. Tatizo lao wameshazoea pesa ya kiingilio na wakurugenzi wa bendi.
 
yaani uupate wimbo wa mbaraka mwinshehe then utake wimbo wa dansi wa 2000 ukose?? sio kweli.

we ulitaka wimbo gani ukaukosa?
Diamond sound-kibinda nkoy(original)album yao ya kwanza.Acha kibinda nkoy remix.
Stono musica album zao zote.
Nina Musica. Ni nyingi bro huwezi zipata mtandaoni.
 
Kaka nimeshafanya sana hivyo.Fanya hivi...ingia youtube search hui wimbo(kibinda nkoyi), screenshot halafu weka hapa.
 
Back
Top Bottom