Kwa Wamiliki wa Toyota na gari zote zinazotumia CVT

Kwa Wamiliki wa Toyota na gari zote zinazotumia CVT

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Toyota anatumia gearbox za aina tatu.

1. A type, ambazo zimefungwa kwenye SUV nyingi kubwa za Toyota. Mfano A343F iliyofungwa kwenye Toyota prado TX 1997.

2. U type, ambazo zimefungwa kwenye gari ndogo nyingi za toyota. Mfano U341E ambayo ipo kwenye NADIA .

3. CVT, ambazo zimefungwa kwenye gari nyingi zinazoanzia mwaka 2007 na ndio gearbox inayofungwa kwenye gari nyingi sasa hivi. Mfano K111F ambayo imefungwa kwenye Noah Voxy ya mwaka 2004.

Hii aina ya tatu ndio hasa nimeilenga.

CVT ni continuous Variable Transmission. Tofauti ya CVT na convetional Automatic Transmission ambazo zipo kwenye gari nyingi ni kwamba CVT inakuwa na pulleys mbili pamoja na mkanda ambao hutengenezwa kwa Steel.

Gearbox ya CVT inamatumizi mazuri ya mafuta sababu nguvu haipotei wakati wa kubadili gear. Gari yenye CVT haina shift points yaani hutakaa uifeel inabidili gears, Utaona tu inaenda, huwa inabadili kimyakimya. Pia CVT inachanganya haraka sana ukiwa barabarani, japo haiifikii DSG transmission.

Sasa gearbox ya CVT inahitaji care ya hali ya juu sana kwa sababu kitendo cha kuweka oil ambayo si yake ndio ushaua gearbox ndani ya muda mfupi tu. Hivyo kama gari yako ina CVT ni vizuri wewe mwenyewe ukawa na uelewa ni oil gani inahitajika kwa gari yako siyo kupeleka tu mahali ubadilishiwe oil kwa sababu utawalaumu. Vinginevyo huko unakopeleka wawe na uelewa wa hizo gearbox.

Pia hizi ni gearbox za gharama sana. Mfano gearbox ya Toyota IST ya mwaka 2007 inauzwa siyo chini ya milioni 2. Oil yake pia ni gharama. Japo ukiweka unatembea mpaka unasahau. Mfano gearbox nyingi za CVT interval ya kubadili CVT fluid ni kuanzia 50,000Km.

Kama una gari ya toyota fungua huko kwenye bonet tafuta kibati huwa kinakuwa na rangi ya silver mara nyingi japo mara mojamoja huwa kinakuwa na rangi nyeusi. Halafu soma sehemu fulani pameandika Trans/Axle hiyo ndio model ya gearbox yako. Mara nyingi huwa inakuwa na herufi mwanzoni, ikifuatiwa na namba zinakuwa tatu halafu sometimes inaweza kumaliziwa na herufi nyingine au isimaliziwe.

IMG-20210108-WA0016.jpg

Sasa ukiona herufi ya mwanzo ni K basi gari yako ina gearbox ya CVT. Jitahidi kuwa makini.

Hizi ni baadhi ya gari za toyota zenye CVT transmission,

Toyota Rumion, Toyota Sienta, Toyota Ist kuanzia 2007, Toyota Vitz kuanzia 2005, Toyota Passo kuanzia 2010, Toyota Ractis, Toyota Crown kuanzia 2008, Toyota Premio kuanzia 2007, Toyota Rav 4 kuanzia 2005, Toyota Noah kuanzia 2004, Toyota Alphard kuanzia 2008, Noah Voxy kuanzia 2004,

Brand zingine zinazotumia CVT kwa kiasi kikubwa ni Nissan, Honda na Subaru.

*******########*********

Car Diagnosis, Engine service, Repair, Check engine, na mengine mengi.

Karibu Ofisini kwetu Dar es salaam, Sinza Kijiweni.

0688 758 625 au 0621 221 606
 
Aisee Acha jumatatu nikupigie simu nije kazini kwako hapo mitaa ya magomeni angalau nipajue Tu hapo ili siku ya kufanya service unichekie kilakitu...
Gear box oil unazo mwenyewe au naweza kuja nayo?
 
Aisee Acha jumatatu nikupigie simu nije kazini kwako hapo mitaa ya magomeni angalau nipajue Tu hapo ili siku ya kufanya service unichekie kilakitu...
Gear box oil unazo mwenyewe au naweza kuja nayo?

Aiseeee karibu. Japo kwa bahati mbaya sihusiki na masuala ya kuuza Oil na kibadili oil kabisa. Hizi thread huwa naziandika tu kwa sababu ni vitu navifahamu na pia kuna matatizo ambayo nakutana nayo kwenye magari ya watu ambayo yanasababishwa na hizi oil.

Kwa sehemu kubwa nafanya Diagnosis pamoja na repairs za mifumo ya umeme kwenye engine, Automatic gearbox, ABS, airbag n.k.
 
Mie ninatatizo la signals za ac nikiwasha aircon.

Inatakiwa ifungue compressor na fan kwa pamoja ila fan inawaka compressor haiwaki.
Mwanzo nilihisi ni gas ila nikajaza upya just to find out kuna shida kwenye control unit. Compressor haiwaki kabisaa. Ila ikiungwa direct inazunguka so ni nzima unaweza kusolve hili tatizo?
 
Sijajua gari yako ni gari gani.

Ila nmewahi kutana na ishu ambayo slightly inafanana na hiyo yako. Ilikuwa ni kwenye Alteza moja hivi.

Kwenye baadhi ya gari wameweka Solar sensors ambazo kazi yake ni kumonitor joto humo ndani kwenye gari na signal yake ndio inaweza kuamua kama Compressor iwake au lah hasa kama unatumia Auto mode.

Sasa hiyo solar sensor ikileta shida inaweza kupelekea shida kama hiyo yako.

Kitu cha msingi ili niweze kuona tatizo kwenye AC inatakiwa gari yako iwe na Control module ya AC ambayo inajitegemea. Kinyume cha hapo siwezi kufanya Diagnosis yoyote kwenye mfumo wa AC.
 
Duh, sasa hii control Module ya AC inakaaga wapi au unaweza kuiona kwa kutazama kwenye bonet ?
Kama ulisolve kwenye

Altezza basi hata yangu hutashindwa maana gari yangu ni Toyota Opa model ya 2003 ile. Pamoja na hizo Altezza si ni gari za kipindi hiko hiko naimani hata mifumo yake itakuwa inaendana endana given its a Toyota
 
Mashine ninayotumia naweza kuscan nikajua gari imekuwa equiped na mifumo ipi na ipi. Sasa mifumo ambayo inaonekana kwenye mashine ni ile tu ambayo ina module zake zinazojitegemea.

Maana mashine inawasiliana na module.

So far Opa ya mwaka huo inaweza ikakubali.
 
Basi itabidi siku nipite maeneo ulipo! Nipe address nijue nakufikiaje
 
Kwenye Ac system, gari zume advance sana, kuna gari zinakuja na normal ac system, na kuna zinakuja na kitu kinaitwa climate control.... Sasa hizi za climate control zinakua na sensor nyingi za kufanya ac system ifanye kazi na zinakuja na compressor ya umeme..

Sasa kwa case ya huyu jamaa labda kwanza aseme ni gari gan na ya mwaka gani anatumia ili aweze kusaidika.

Ingawa pia kasema akiunga direct compressor inafanya kazi(hii maana yake ni kwamba gari yake inatumia compressor yenye clutch ya nje) sasa kama inabana kwa direct unaweza cheki fuse ya clutch na relay yake, na ac pressure sensors pia (usiwe ume modefy compressor kutoka ya umeme kwenda ya external clutch maana kama ume-modefy the approach to the problem can be different)
 
Car Diagnosis, Engine service, Repair, Check engine, na mengine mengi.

Karibu Ofisini kwetu Dar es salaam, Sinza Kijiweni.

0688 758 625 au 0621 221 606
 
Nafikiri JamiiForums wangeanza kucompensate users wenye most useful contents. Huwezi linganisha haya madini na jinsi ya kula tunda kimasihara, tuseme tu ukweli.
 
Back
Top Bottom