Kwa wanafunzi wa vyuo vikuu tu

jorojo

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
1,642
Reaction score
11
Vijana wenzangu hasa wa vyuo vikuu na huu ni waraka wangu kwenu nahisi huu ni wakati wa kubadilika kifikra na kimtazamo mara nyingi nimepita humu jukwaani nakuta mabishano ya kipuuzi eti chuo gani bora huu ni ujinga nadhani ni vyema mngeonganisha mawazo yenu na kujadili ni njia ipi itumike kuwapa elimu ili jumuiya ya Africa mashariki ikipamba moto iwe nafuu kwenu kushindana na wasomi toka Kenya,Rwanda na Uganda maana kwa sasa tunachemka sana na si kubaki na mambo ya kipuuzi kiukweli hatutafika tubadilike na tuheshimiane. Sisi ni watu muhimu sana kwa maendeleo ya nchi hii huu si mda wa kujihisi sisi ni watoto sisi ni watu wazima hayo mambo tunayoyafanya ni ya kitoto ebu tujaribu kufikiria maendeleo ya nchi hii naamini huu ni waraka wa mabadiliko tubadilike. MUNGU WABARIKI WANAOTAKA KUBARIKIWA
 
Hao unao wasema watakuja sasa hivi subiri usishangae wakakwambia ww utakuwa unasoma TMBI sjui ITA ndomana umeandika hivi
 
Umenena kweli post nyingi za kijinga ni wanavyuo wanazitupia tena baada ya kununua kasmart ka tigo promo kifurushi mwaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…