comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
“Walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakayokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” (Mwa.2:17).
Shetani alidai “Hakika hamtakufa.” (Mwa. 3:4).
Lakini baada ya kutokutii, Adamu na Hawa waligundua kuwa mshahara wa dhambi kwa uhalisi ni “mauti” (Rum.6:23).
Hukumu yao ilibeba maneno haya:
“kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.”(Mwa.3:19)
-----
Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Geita, Fravian Kasala amesema watu wanatakiwa kutokuwa na wasiwasi kuhusu kifo na kinapotokea watambue kuwa ni mpango wa Mungu.
Ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Februari 6, 2021 katika ibada ya mazishi ya aliyekuwa katibu tawala wa Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega iliyofanyika kijiji cha Ngoma Wilayani Sengerema katika kanisa la Mtakatifu Benerdicto.
Amesema kifo cha Kwitega ni mwanzo mpya wa maisha yake mbinguni, “tunapaswa kumwombea na tuyaenzi yote aliyofanya hapa dunia kwa kuwa ameacha alama isiyofutika katika utumishi wake wa umma.”
"Tusali kila siku hatujui siku wala saa ya kuondoka hapa duniani. Maombolezo haya ya leo yasiwe ya kukata tamaa, yalete tumaini jipya kwa mwanadamu. Mwanzo wa kufa ni mwanzo wa maisha mema huko mbinguni, “ amesema Askofu Kasala.
Kwitega alifariki Februari 3, 2021 katika ajali wakati akitoka Arusha kwenda Dodoma baada ya gari alilokuwa amepanda kugongana uso kwa uso na basi. Katika ajali hiyo watu wanne walijeruhiwa ambao ni dereva wake na wanawake watatu waliokuwa kwenye basi hilo.
Chanzo: Mwananchi