HATUA ILI UWEZE KUPIMIWA KIWANJA AU SHAMBA LAKO (Ili uweze kupata hati miliki)
[emoji637] Ukaguzi wa eneo lako husika ili kujua eneo lako limepangwa kwa ajili ya matumizi gani, Hapa atashirikishwa mpima ardhi kwa ajili ya kufanya utambuzi wa eneo husika kujua lipo kwa ajili ya matumizi gani, Hivyo ni lazima afike site kwako na kifaa (Handheld GPS), Achukue vipimo kuzunguka eneo lako, Baada ya hapo akatafute taarifa za eneo lako halmashaur/ wizaran ili aweze kupata raman ya mipango miji.
[emoji638] Matokeo ya zoezi la ukaguzi wa eneo,
[emoji654] Eneo husika kukosa sifa za kupimika, eneo husika linaweza likakosa sifa za kupimika kwa eneo husika kutokua limeandaliwa matumizi kabisa (halina mchoro wa mipango miji), Eneo husika kuwa lipo katika matumizi ya maeneo ya kijamii mf makabuli, barabara, soko n.k
[emoji654] Eneo husika kuwa na sifa ya kupimika,
Eneo husika kuwa katika matumizi ambayo mtu binafsi anaweza kumili mf makazi, hotel, biashara n.k
[emoji639] Kibali cha upimaji,
Mteja au mmiliki halali wa eneo husika inabidi aandae barua kwa ajili ya kuomba kupimiwa eneo lake, Barua hiyo itapita serikali ya mtaa na halmashauri husika.
[emoji640].Upimaji,
Hapa ni suala la kitaaluma zaidi ambapo mtaalama ataweka mipaka katika eneo lako kwa kutumia mawe (beacons), litaandaliwa file kwa ajili ya kwenda wizaran likiambatanishwa na ramani ya upimaji. Na mwishowe utarudishiwa ramani iliyo hakikiwa toka wizarani kama ramani ya upimaji.
[emoji641] Mteja utakabiziwa ramani ya upimaji,
ambayo utapaswa uende nayo kwenye halmashaur husika umuone afisa ardhi ili aweze kukuandalia hati miliki yako.
[emoji642] Gharama za upimaji zinatokana na ukubwa wa kazi yaan idad ya ekari na viwanja hivyo inaweza kuwa laki3, 5,6,7 ...hadi 2m itategemea na idad ya viwanja.
By Surveyor Aloyce
WhattsApp 0713778937
[emoji338] 0754619189
[emoji338] 0686087101
GOLD LAND CONSULT CO. LTD
Tunapatikana Sinza legho