King Kong III inategemea ni wapi. Kama ni karibu na kiwanda na ni katika njia kubwa (Main Road) bei ni hizo na hata zaidi. Ila kama ni ndani kidogo bei ni poa sana. Huko ndani kidogo waweza kununua kila eka hata 150,000/=.
Nilishangaa sana nilipokwenda Msanga (kama 60km toka Kisarawe) ambapo nilikuta akina Mangi tayari wamekwishajiwahi. Ukiuliza hapa vipi unaambiwa hapa ni kwa mangi fulani n.k. Kwa hiyo watu (hasa toka town) tayari wamekamata na wanasikilizia tu kuongezeka kwa infrastructure waanze vitu vyao.