Nashauri msimpotoshe mleta mada, hizo product zina ubora mzuri na kampuni zote tatu GNLD, Forever Living na 4Life wanafanya biashara ya Network Marketing na si Pyramid Scheme.
Tofauti ya MLM (Multi Level Marketing) kulinganisha na Pyramid Scheme ni kuwa ili uweze kufaidika na hayo 'mamilioni' lazima ufanye kazi inayoonekana (kutokana na taratibu za WAZI kampuni ilizojiwekea), faida hiyo ni sehemu tu ya pesa ulizotengeneza katika biashara ya jumla (aidha kwa kuuza bidhaa, kuingiza watu wapya au kutumia binafsi) na inapanda na kushuka kutokana na juhudi yako ya biashara ya kila siku. Katika MLM hakuna kulala nyumbani miezi sita bila kufanya kazi halafu utengeneze pesa, unatengeneza kulingana na kazi uliyofanya. MLM haiangalii nani kaanza mwanzo bali yule anayefanya kazi kwa bidii kuitengenezea kampuni husika biashara.
'Pyramid Scheme' ni tofauti maana inashawishi uingize pesa mwanzo halafu ukachape usingizi ukisubiri pesa, na faida yake inaangalia aliyewahi mwanzo na wengine wote wanaoingia baadaye ni kumtajirisha wa mwanzo au aliye juu.
Nashauri msome zaidi ili kutofautisha hizi biashara mbili.