Kwa wanaoijua shato pori (SP) nimeiaplai leo

Seneta Wa Mtwiz

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2013
Posts
3,635
Reaction score
4,160
[emoji121]
Wakuu

Leo nimegundua kumbe ile kozi ya *sp_319 (shato_pori)* niliyoipiga kwa vitendo kutoka mabibo_hostel hadi mlimani_main_campus nikiwa chuoni ina umuhimu mkubwa sana
Hasa katika kipindi hiki nyeti cha kusubiria ajira zetu.

Kumbe kutoka *simu2000* mpaka *bunju_b kwa yong'eyong'e*
Sio mbali hata kidogo.

Baada ya kupiga mahesabu ya buku yangu iliyobakia mfukoni
Na kugundua kuwa nikitoa 500/= ya nauli
Yabidi nisahau kuhusu mlo wa usiku,
Basi leo nimetembea kwa miguu kutoka *mawasiliano* hadi *bunju b*
Na nikaona kawaida tu!

Ushauri wa bure:

Hii kozi ya *shato_pori 319*
Iwe ni ya lazima vyuoni
Kuanzia mwaka wa kwanza hadi wa mwisho.

Kwani ina msaada mkubwa sana katika kipindi kigumu kiuchumi.
-------

Na nadhani hata ile intavyuu niliyoitwa alhamisi *babati*,
Nikikurupuka zangu j.5 alfajiri kwa staili ya jogging,
Kufikia saa kumi na moja jioni nitakuwa eneo la tukio kusubiria intavyuu.

Na ni kwa nia tu marafiki.
 
All the best hofu yangu usije ukafikia hospital.. Nimecheka sana... Kweli nimeamini ugumu wa maisha kipimo cha akili
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] festi yia kipindi natoka jeshini jkt mwili bado una manguvu niliipiga sana hii kitu, miaka miwili iliyofuata nikaachana nayo kabisa.
 
Hahahaha!!!Shattle pori!!nilii apply sana enzi hizooo!!boom ikikata shuttle pori ndo mambo yote
 
Hahahahaha kweli ugumu wa maisha ni kipimo cha akili
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] festi yia kipindi natoka jeshini jkt mwili bado una manguvu niliipiga sana hii kitu, miaka miwili iliyofuata nikaachana nayo kabisa.
Kumbe tulikuwa wengii kipindi hicho tumetoka 824 but second year nkaanza kusahau hizo mambo
 
C mlikuwa mnasema tunaogopa foleni kumbe kulikuwa kufulia
 
Hii kitu niliipiga miaka yote mitatu pale bibo,hadi nikazoeana na wale chinga wa pale darajani.ud unatoka na degree 700 asee.
 
Tulipiga sana shato pori via geti maji enzi za ujana wetu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…