Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nina shamba la ekari moja na robo eneo la Iwambi nataka nizungushie ukuta gharama ya huo ujenzi inaweza cost sh ngapi? najua cement haitoitajika wala mchanga hapo ni mafundi tu. wakazi wa mbeya msaada.
Hilo swali laweza jibiwa na fundi yoyote hapa Tanzania!
Siyo kweli mkuu.
Ingekuwa hivyo hata kodi za vyumba na nyumba zingekuwa moja nchi nzima.
Mzunguko wa pesa na upatikanaji wa hitaji hupelekea bei ya kitu husika.
Aina ya mafundi unaohitaji ni ipi mkuu?
1 wa mtaani
2 madalali
3 kampuni.
Ufafanuzi:
Wa mtaani anakuwa ni mmoja na kibarua wake. Siku kazi ikimuelemea anaalika mwenzie mmoja. Mpaka kazi itakapoisha.
Madalali anaalika mafundi wengi wazuri anaowajua yeye anakupigia kazi kama hiyo kwa siku tatu tu.
Kampuni ndo kama ujuavyo. Zipo kampuni ndogo ndogo nyingi mjini hapa zinazijishughulisha na ishu hizo.
Lakini pia watataka kujua aina ya tofali utakazo tumia. Kama ni za kuchoma au za block.
I can give you their contacts.
Hongera kwa kumiliki 'gujieneo gukubwa namna hiyo mjini'
Swali lako halijakamilika
-matofali unayo
-kama huna ni ainagani na unayapataje, mfano ya kuchoma kuanzia Tsh 120 mpaka 140 kupakia, kubeba na kupakuwa haijajumuishwa
-huhitaji cement, udongo utaupataje
-mchanga unao una uptaje mfano lori la saizi ya kati-fuso ni kati ya Tsh 70,000 mpaka 80,000 gharama zote-upakiaji,usafishaji na kushusha
-mbao kidogo za kusimamia mafundi kama uzio utapanda juu kidogo inaweza kukosti Kati ya 30,000 mpaka laki moja kulingana na mhitaji
-maji yanapatikanaje
-mafundi mfano Tsh 15,000 mpaka 25,000 kwa siku kulingana na ubora wao, wanajenga urefugani kwa siku niusimamizi wako au makubaliano yenu
-wasaidizi mfano 5000/day
Kaa chini ufanye upembzi yakinifu kisha fanya maamuzi kulingana na fungu lako la fedha kukidhi malengo yako.
nina shamba la ekari moja na robo eneo la Iwambi nataka nizungushie ukuta gharama ya huo ujenzi inaweza cost sh ngapi? najua cement haitoitajika wala mchanga hapo ni mafundi tu. wakazi wa mbeya msaada.
ina maana tofali unazo tayari? na kama ni tofali za kuchoma ina maana unataka ujengee tope?
Kwa hiyo unahitaji fundi tu. wewe uko mbeya au hauko huko?
Njia rahisi ni hii: Tafuta fundi (kama unataka kubana matumizi achana na kampuni wanataka faida na wao), tafuta mafundi hata watatu au wanne (pesa ni ileile kwa sababu unawalipa kwa siku), unaelewana nao wanapiga kazi, kuwa mkali na mikwara mingi kila mtu amalize ukuta wake ndani ya muda na kwa kiwango cha kuridhisha (usimamizi muhimu). Kupata fundi mzuri kama wewe si mwenyeji tembelea maeneo yenye ujenzi unaoendelea, ongea na mafundi mbalimbali watakupa mafundi tena wanakuonesha kabisa fundi fulani amejenga paleee, kinachobaki ni maelewano "padiem",yeye ataita vibarua wake kazi inaanza.
Umeilewa mada vizuri?
Kama umeilewa nipe fact in issue hapo, then uniambie ni vipi fundi asiekaa mbeya anaweza kushindwa kutatua issue hiyo?
ina maana tofali unazo tayari? na kama ni tofali za kuchoma ina maana unataka ujengee tope?
Kwa hiyo unahitaji fundi tu. wewe uko mbeya au hauko huko?
Njia rahisi ni hii: Tafuta fundi (kama unataka kubana matumizi achana na kampuni wanataka faida na wao), tafuta mafundi hata watatu au wanne (pesa ni ileile kwa sababu unawalipa kwa siku), unaelewana nao wanapiga kazi, kuwa mkali na mikwara mingi kila mtu amalize ukuta wake ndani ya muda na kwa kiwango cha kuridhisha (usimamizi muhimu). Kupata fundi mzuri kama wewe si mwenyeji tembelea maeneo yenye ujenzi unaoendelea, ongea na mafundi mbalimbali watakupa mafundi tena wanakuonesha kabisa fundi fulani amejenga paleee, kinachobaki ni maelewano "padiem",yeye ataita vibarua wake kazi inaanza.
Kwa uzoefu wangu wakuu naona madalali ni wazuri.
Fundi anakuwa na tenda nyingi.
Atakuja anajenga siku moja anachukua advance anaondoka humuoni siku mbili au tatu.
Yaani kazi ya siku tatu itafanyika mwezi.
Harafu akifika kati lazima atakubembeleza kuwa alikosea mahesabu hivyo anaomba umuongezee kiasi kadhaa.
Yaani huwa inakera sana.
Nimekutumia # mkuu.nimeku-PM