Nadhani mnashindwa kuelewa jambo moja. Wakati mnafunga ndoa iwe kanisani, bomani au kwa shehe, kile cheti kuna sehemu wameandika, Je ni ndoa ya mke mmoja au wake wengi? haijaandikwa, Je ni ndoa ya mume mmoja au waume wengi? Mke na mume wote wanadelete sehemu isiyotakiwa. Kama wewe mwanamke unakubali mwenyewe ndoa ya wake wengi, sasa tatizo ni nini? Kama hukubali basi pale pale, andika ndoa ya mke mmoja tu! tatizo inawezekana wanawake wengi sijui ni kimuhemuhe cha kuolewa, wao wanadelete tu bila kujali, halafu jamaa akija nataka kuoa wa pili unakuja juu!