Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

BradFord93

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2017
Posts
917
Reaction score
2,217
Kumekuwa na malumbano kuwa biashara ya duka hasa rejareja haina faida. Leo nitaleta baadhi ya bidhaa tu kupinga malumbano hayo (maana ndo ishu nnayoifanya)

Just kabla sijaanza, ukitaka kuona mafanikio ya hii biashara wewe muuzaji uwe mtaji wa kwanza. Kichwa chako kiwe mtaji dukani pia mazoea kwenye duka pamoja na mahusiano ya kimapenzi weka pembeni kabisa

1. Soda
Pepsi huuza kreti kwa sasa 9500(soda jumla hua 24 kwenye kreti). Ukiuza jumla utapata 12,000 (faida hua ni 2500)
Coca wanauza 10,000(hapa faida 2000). Take away zinauzwa katon 9,000 na znakuwa 12 (faida 3,000)

2. Vocha
Hapa nazungumzia za kurusha, za kukwangua sincerely speaking sijawahi kuuza na sitarajii.

- Tigo hutoa 6% kama faida kwa kila float utakayonunua (ukinunua float 10,000 unapata 600 (hapa bado faida za kwenye vifurushi). Ukiunganisha internet ya buku kwenye float wanakata 900 mteja atakupa 1,000..100 ya kwako

Voda hutoa 8% kila unaponunua float (ukinunua float 10,000 unapewa 800 (hapo pia kuna faida ukiunganisha vifurushi)

3. Maji makubwa Uhai
Lita 6 unanunua yakiwa matano kwa 8500 utauza kwa elfu 2 jumla unapata 10,000 (1,500 ya kwako)

Lita 12 unanunua kila moja 2500 utauza kwa 3,500 (1,000 kila dumu moja ni ya kwako)

4. Viberiti unanunua dazeni 4,500 unapata 9,000 (4,500 ya kwako)

5. Pampers unanunua 14,000, zinakuwa 40(kila moja utauza 500. Unapata 20,000 (elfu 6,000 ya kwako)

6. Sabuni ya unga ya kufunga
Utanunua kiroba elfu 31,000. Ukifunga vizuri na kwa kipimo cha 500 (faida mpaka 10,000 unapata)

Kuna vingi vya kuweka ila sitamaliza leo. Hapo bado sijataja unga, mchele, sukari, ngano, maharage, omato na vingne kibaaao

Hakuna biashara mbaya, ni wewe mfanyabiashara. Msimamo wako na unavyoichukulia biashara yako

Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi, kreti la coca, paketi za sigara, pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama.

Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimefanya sana hiyo biashara pale Mlandizi jirani na Bar ya Kauli ya Bibi, kikubwa ni lazima ukae mwenyewe dukani au mkeo, vinginevyo utapigwa tu. Mimi nilikosa usimamizi sababu naishi Kimara kazi nafanya mjini, kule nakwenda wikendi tu, mwisho wa siku nikaamua kuliuza duka kwa jamaa.

Lakini ukweli ni kwamba inalipa sana ukiwa mwenyewe, pia niliweka na vibia viwili basi mwendo ulikuwa oya oya tu.
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi,kreti la coca,paketi za sigara,pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama. Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Sana kiongozi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hizi bidhaa unaziuza kwa muda gani? soda crate 1 unauza wiki 2, muda huo umeshatumia zaidi ya 20k faida iko wap
Inategemea na mzunguko wako. Ukiuza soda pia uwe na friji zuri, wateja hupenda soda zile baridi kweli ndo hua nnachowakamatia hapo nina kreti sita, ila ndan ya siku 2 kreti 3 tyr zmeisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi,kreti la coca,paketi za sigara,pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama. Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo maana ikawepo hela ya biashara na ya mtu bnafsi, fanya huo upuuzi wote lkn isiwe kwa hela ya dukan. Heshima ya pesa kwenye biashara n kitu muhim saana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kumbuka siku ukinywa bia kama tano ni 2000 X 5= 10,000/: ukila na kitimoto kilo moja na ndizi ni 12,000/: hapo utakua na demu nae atakunywa santiana au dompo 15,000/: ukitoka hapo ingia gesti ya bei rahisi ya 20,000/: mtoe demu asibuhi na hata 20,000/: utakuta umekula creti la pepsi,kreti la coca,paketi za sigara,pampers zisizohesabika, viberiti mabunda kadhaa nk. Kazi ya kuuza duka hata ukila mchana ujue shelfu itakutizama. Munisamehe

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji2] [emoji2] [emoji2]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mm nimeifanya 2011..kwakweli faida yake ndg..ss hv ht nipewe5m hii biashara siirudii, sukari mfuko unanengeneka for 2 wks upate 7500😂😂😂sitaki..

Ngano faida ilikuwa km 6000 bas uishe ht 2 days😏 unakaa nao week na nusu😑

Vinywaji ndo vinabeba duka
 
Inategemea na mzunguko wako.....ukiuza soda pia uwe na friji zuri...wateja hupenda soda zile baridi kweli...ndo hua nnachowakamatia hapo...nina kreti sita....ila ndan ya siku 2 kreti 3 tyr zmeisha

Sent using Jamii Forums mobile app
Hongera mpendwa !! Hapo nakuombea uzidishiwe na uwe na nguvu ya kuto kula ktk mtaji wa duka for 2 years !!
InshaAllah utaleta marejesho Muruwah!!
 
mm nimeifanya 2011..kwakweli faida yake ndg..ss hv ht nipewe5m hii biashara siirudii...sukari mfuko unanengeneka for 2 wks upate 7500[emoji23][emoji23][emoji23]sitaki..

ngano faida ilikuwa km 6000 bas uishe ht 2 days[emoji57] unakaa nao week na nusu[emoji58]

vinywaji ndo vinabeba duka
Tatzo n focus ndugu. Vitu vnavyotoka kwa wingi ndo vikazanie, vingne n kuvutia wateja, mfano mimi kwakwe nnachouza saaaana n soda na vinywaji vngne ukimalizia n vocha na huduma za mobile banking. Biashara hii inahitaji focus mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom