Kwa wanaosema biashara ya duka haina faida, soma hapa tafadhali

Unafanya biashara gani?
 
we jamaa fala sana
 
Show zipi ni za kibabe unaweza kuja 500k kwa wiki boss?
 
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nimesoma comments za watu wote humu. Wengine wamekomenti ila bila kujua au kufanya hii biashara. Biashara hii ukikaa sehemu nzuri, mtaji mzuri angalau 7M mpaka 10M na ukawa na mauzo yasiyopungua laki 3 mpaka 5 kwa siku. Na upo serious ucheki na wateja. Lazima utoboe.

Hawa wanaokatisha tamaa itakua location haikua nzuri ama mtaji ulikua mdogo sana. Au biashara siyo asili yao. Hivi vitu biashara zina wenyewe. Ndiyo maana kuna watu wanaanza na mtaji wa matunda baadae wamemiliki biashara kubwa ssana.Wanajua kuzidisha ela. Siyo watu wote wanajua hizi mambo. Ndiyo maana wachache wanamiliki pesa. Kwa mtaji huo juu, na mauzo hayo juu tayari ndani ya miezi michache unaweza kuanza kununua vitu kwa wingi na ukaanza kuwa na store ya kuhifadhi mizigo. Ndani ya miaka 3 hivi utajikuta una mzigo dukani wakutosha na store mzigo wa kutosha utafikiri umeletewa kimiujiza.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ulianza na mtaji kiasi gani mkuu? Ongea ili vijana wapate nguvu kwa walichonacho
 
Kila biashara na watu wake, mimi nafanya hii biashara nina duka la nafaka, ila kabla ya hapo nilikuwa nafuata mzigo wa mchele na maharage mbeya na iringa nauza kwa jumla. Nikaacha niliona miyeyusho maana sometimes nilikuwa naleta mchele unakaa wee wakati mimi nataka niuze week uishe nifuate mwingine. Niliona kama nimetia pesa nyingi, nguvu nyingi mapato kidogo, halafu sasa nikawa nasupply maharage shule flani baadae wakaanza nizungusha malipo ndipo nikaona hii biashara niachane nayo.
Hata hili duka nimeliacha likue tu nauza kuanzia kilo tano kwa kila aina ya nafaka.
 
Wadau ili kupata mrejesho mzuri ni bora kununua vitu kwa wingi mfano katoni au kidogo kidogo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…