Kwa wanaotaka kusoma nje ya nchi

Wewe hautatulipa chochote mpaka upate viza nasi tutalipwa na chuo

Chuo kitawalipa kivipi?

Mmefanya arrangements na hivyo vyuo kuwalipa kwa kuwatafutia wananafunzi?

If so, mnaweza kutupa list ya vyuo ambavyo mmeingia navyo ubia ili potental stundents waweze kufanya verifications kama kweli hizo arrangements zipo?
 
all the best katika kazi yako ila ukweli halisi mkuu ma agent wengi huwa si wa kweli kwenye kumuambia mtu ukweli uhalisia wa maisha ya nje najua mmeingia mkataba na vyuo mbalimbali mwanafunzi akipata visa tu nyie mnapokea chenu, iila kwa upande wa wanafunzi jamani siku hizi kusoma nje unatakiwa uwe na pesa ya kujikimu kabisaa hasa kwenye nchi ya uk sijui nchi nyingine kama USA na Canada hawa ma agent huwa wanawaambia ukilipa tu advance payment ya fees ukienda kule unapata kazi wala hakuna shida unaanza kuingiza pesa, kumbe wao wanataka ulipe upate admission na visa wanakuambia omba hela kwa mjomba au shangazi kusanya kwenye bank yako hela zikifikia kile kiwango ambacho visa requirement inavyosema cas letter yako visa inatoka na visa ikitoka tu agent hapo anaingiza chake sasa mtihani unabaki kwa mwanafunzi anaondoka masikini na nauli labda na hela ndogo sana mategemeo yake anajua atafika tu atapata kazi ilingali na huku nyuma ndugu zake wanafikiria akifika ulaya tu ataanza kututumia iphone, sijui vi perfume, mwanafunzi anakutana na kitu kisichohalisi, jamani tuwe tunawaambia ukweli nchi hii sasa imejaa wapoland, romanian, na wengine wote wananjaa kuliko hata black kutoka africa ajira sasa ni shida tupu vile visahani tuliokuwa tunavisafisha havipo tena sio zamani mtu alikuwa anakuja na pound 2000 tu mtu anamaliza shule maana kazi zilikuwepo siku hizi unatakiwa kuja full kifedha, maisha yamebadilika sana sana inabidi tuwe wa kweli kuliko kufikiria kuingiza pesa tu ilingali tunawaacha watoto wa watu katika mateso, hili nina uzoefu nalo kabisa kuna agent mmoja yupo hapo posta dar kamwambia kijana wa watu wewe lipa 50% ya school fees mambo mengine utayapata huko, uzuri kaka yake nafahamiana nae akaniuliza nikamuambia ni uongo nilimpa ukweli mtupu jamaa akarudi kuwaeleza walimjibu eti mimi sijui kitu nina wivu tu wao wamekaaa huku miaka 10 nikasema sawa endeleeni visa imetoka jamaa kuja alipangiwa chuo maeneo ya birmingham sisemi ni chuo gani kufika tu anatakiwa alipie chumba si chini ya six month jamaa ana pound 300 tu mfukoni nikaanza kusumbuliwa na simu ooh kuna mdogo wangu kakwama sio siri nilimjibu niko na maandalizi ya kurudi nyumbani bongo na cha msingi ni pesa hakuna kiingine tumeni pesa ukweli jamaa wakichofanya ni kumtumia nauli ya kurudi na wakapoteza £4300 waliokuwa wameilipa, ni hasara kubwa kwa mtanzania, ukweli siku zote utatufanya tuwe huru na amani kuliko kupokea pesa ya mtu ilingali unaju ni udanganyifu, ni mara mia kuwasiliana na wenye chuo moja kwa moja sema watanzania tunaogopa sana, nilishangaa sana hata visa eti ya kwenda india/dubai mtu anapitia kwa agent wakati unaweza kwenda pale moja kwa moja kupata info zote zinazotakiwa. hata ticket ya ndege jamani?? huu ni uvivu uliokithiri.
 
nataka nianze kukuelewa kuwa wewe utalipwa na chuo, ila ulikosea sana kusema kuwa hutanicharge chochote nikastuka kidogo kwa vya bure navyo vina utata!!!! kama kipindi kile ile DECI ilikuwa unapanda mbegu zako the inadabo ndani ya muda mfupi na pipo hawakushtuka
 
Chuo kitawalipa kivipi?

Mmefanya arrangements na hivyo vyuo kuwalipa kwa kuwatafutia wananafunzi?

If so, mnaweza kutupa list ya vyuo ambavyo mmeingia navyo ubia ili potental stundents waweze kufanya verifications kama kweli hizo arrangements zipo?

naweza nitakuwekea list yote ili ufanye verification kwa sasa natumia cm so usijaj juu ya hilo
 
siwezi pata full ufadhili.!maana sina hata sh.mia ya kuanzia kama air ticket.,malazi huko e.t.c nifafanulie,umaskini huu.!

Kama una good pasng marks njoo ofisini tutakusaidia kwa ushauri on what 2 do ila uwe fit kichwan koz kuna mitihan
 
Kama una good pasng marks njoo ofisini tutakusaidia kwa ushauri on what 2 do ila uwe fit kichwan koz kuna mitihan

good passing maksi ndo zipi? Mbona uko brief sana utafikiri unaandika shortnotes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…