Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,169
- 3,351
Kabla ya mtu kuoa au kuolewa ni lazima anakuwa na vigezo vyake lakini mara baada ya kuanza maisha wengine hugundua kuwa aidha walikuwa sahihi au siyo sahihi kipindi walipotoa ridhaa zao na kwa sababu tayari wanakuwa katika ndoa inakuwa ngumu kuachana kwa sababu ndogo ndogo.
Swali? Kama ikitokea watu wakapewa nafasi ya kuoa/kuolewa tena baada ya kuwa katika ndoa aidha ya kidini, kimila au kiserikali ni wangapi ambao wangechagua kuishi na wenzi wao wa sasa?
Naomba kuwakilisha kwa majadiliano.
Hapa suala nafikiri si kukosea, bali ni hulka ya binadamu kupenda kitu kipya. Kwa mfano ukinunua gari jipya ukalitumia kwa miaka 3, lazima utagundua kuwa mtaani au katika soko kuna magari mapya ambayo ni mazuri kuliko lako, na bei zinaweza kuwa zinafanana. Kitendo cha kufikiri kuwa kitu fulani ni kizuri kuliko ulichonacho sasa haimaanishi kuwa ulikosea kununua hicho ulichonacho, bali ni suala la wakati.
Ili kudhibiti hali hiyo, maisha ya ndoa inabidi yalindwe kwa taratibu ambazo ni tofauti na hulka za binadamu, hiyo ndo changamoto ya ndoa
Wazungu wameliona hilo, na wanazingatia wakati wanaoana. Wanafunga ndoa ya mkataba. mfano tutakaa pamoja miaka 3, baada ya hapo tutaangalia tuendelee au tusiendelee
Mfano uholanzi, ujerumani, ubelgiji, ufaransa watu wana register marriage inayotambulika kama 'staying together' Hivyo wanaishi pamoja kama mke na mume, lakini kimsingi hiyo siyo ndoa, ni makubaliano tu ya hao watu kukaa pamoja na kutambuliwa na mamlaka husika. Wakichoka kila mtu anaanza, hakuna kudaiana kitu
Nakubaliana nawe dada yangu Rose lakini unaweza ukanijuza japo skeleton sababu za mke/mme kutokukubali kuishi na wenza wao?apana
asilimia tisini hawatapenda kuish na wake/waume zao
Ukiolewa au kuoa mara ya pili - things will never be the same!!! Kubali au kataa ukweli ndiyo huo...
Watafiti wa mambo ya mahusiano wanaandika hivi "...Kama mwanaume au mwanamke aliyeacha/aliyachwa angepewa nafasi ya kumrudia mwezi wake baada ya muda, asilimia 95% wangefanya hivyo..."
Walio wengi huwa wanapata kuishi kwa taabu katika mahusiano ya pili - it is more or less of "sogea tuishi"!
Mzee wa Rula hii comment ilitolewa jana kwenye thread fulani
Mzee wa Rula kama mtu kaoa au kaolewa kimakosa nadhani hizo ndo ndoa zisizotarajiwa ndo maana unashauriwa kukaa na mpenzi wako kama bf au gf kwa muda fulani, ila ndugu zetu Waislam naona hiyo ingewafaa zaidi maana wao more than one mke wanaruhusiwa....KUMBUKA UKIMWI PIA mtu wangu....
[/B]
Thread gani DA? Naanza kupata na mshituko kidogo maana kuna thread nyingine kwenye jukwaa la MK mnimeitoa baadae leo nimeona thread nyingine yenye picha mbili kama zile tena ya tarehe ya nyuma kabla ya kwangu!!!!
Hiyo inawezekana kabisa pamoja na kuzoeana, yaani watu wanapunguza ubunifu tena. Naunga mkono hoja ndiiii kwa kukonga hapo juu useful post mkuu.Kwa mtazamo wangu haya yote ya kufikiria kupata nafasi ya pili ya kuoa au kuolewa tena yanatokana na wanandoa kujisahau mara tu ya kuoa/kuolewa kwa maana mara baada ya ndoa yale mambo mazuri mliyokuwa mnafanyiana yanapotea na kila mtu anajidai yupo bize na kazi na shughuli nyingine! Inakuwa kama alichokuwa anakitafuta kwa muda mrefu keshakipata so anaona hana haja tena ya kudedicate muda wake kwa mwenza wake.
muda wa uchumba ni miezi 6 mpaka miaka 2 (hii ni kama probation) zaidi ya hapo msifunge ndoa. Pia kama hafai mwambie ukweli unifai kwa sababu 1,2,3. ili wote muwe na amani. Ila ukweli ni muhimu sana na mwanaume lazima ujuwe ku-probe. Pia kuoa ni kama ut-toss dice, unaweza kuona umekosea na kuoa mwingine halafu utakuta bora hata yule wa mwanzo - yaani ni sawa na situation ya 'kuruka mkojo kukanyaga mavi'.
Nimeiona DA ila ina utofauti na hii yangu. Yangu mimi ipo kinadharia sana, yaani mme/mke ambaye yupo katika ndoa hajaacha wala kuachika ila wamekaa muda kidogo baada ya kuoana kama wakipewa nafasi je wanaweza kukubali kuishi na wenzi wao kama maoni yao au wangesema tofauti? Nadhani kama sijaeleweka, nieleweke hivyo.Ile inaitwa "Wasichana wa JF ambao hamjaolewa" Kasome utaikuta
muda wa uchumba ni miezi 6 mpaka miaka 2 (hii ni kama probation) zaidi ya hapo msifunge ndoa. Pia kama hafai mwambie ukweli unifai kwa sababu 1,2,3. ili wote muwe na amani. Ila ukweli ni muhimu sana na mwanaume lazima ujuwe ku-probe. Pia kuoa ni kama ut-toss dice, unaweza kuona umekosea na kuoa mwingine halafu utakuta bora hata yule wa mwanzo - yaani ni sawa na situation ya 'kuruka mkojo kukanyaga mavi'.
Ukiolewa au kuoa mara ya pili - things will never be the same!!! Kubali au kataa ukweli ndiyo huo...
Watafiti wa mambo ya mahusiano wanaandika hivi "...Kama mwanaume au mwanamke aliyeacha/aliyachwa angepewa nafasi ya kumrudia mwezi wake baada ya muda, asilimia 95% wangefanya hivyo..."
Walio wengi huwa wanapata kuishi kwa taabu katika mahusiano ya pili - it is more or less of "sogea tuishi"!
Mzee wa Rula hii comment ilitolewa jana kwenye thread fulani
Upo juu baba nami namuunga mkono huyo shemeji yetu tayari kesha kujua mapungufu yako na kuyakubali.Ndio maana shemeji/wifi yenu amechagua kuendelea nami pamoja na mapungufu yote niliyonayo!