LGE2024 Kwa Wanawake: Una mipango ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu? Kwanini?

LGE2024 Kwa Wanawake: Una mipango ya kugombea katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu? Kwanini?

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Wanawake wa Tanzania, je, umejipanga kugombea nafasi yoyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu ujao?

Ni sababu zipi zinakuchochea kugombea au zinakuzuia?

Ni kweli Wanawake wanaogopa kujihusisha na Siasa au kugombea nafasi za Uchaguzi?

Kwa muda mrefu, kumekuwepo na mtazamo potofu kwamba siasa ni kwa wanaume pekee, lakini wanawake wengi wameonyesha uwezo wa kipekee katika kuleta mabadiliko makubwa kwenye uongozi.

Ni muhimu tushirikiane kuondoa mitazamo hii potofu: Nafasi za kisiasa ni za kila mtu—wanawake na wanaume. Kila mmoja ana nafasi muhimu ya kuchangia katika kujenga jamii yenye usawa.

Kushiriki katika siasa kunatoa fursa kwa wanawake kuongeza kujiamini, kugombea nafasi za uongozi, na kuhakikisha sauti zao zinasikika.

Pia soma: Kuelekea 2025 - Tufanye nini ili kuongeza ushiriki wa wanawake hasa vijana kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
 
Kwa uchumi gani huo? Maana bila vibunda vya kuhonga wajumbe mtu hatoboi, unadhani wanawake na vijana wana nafasi ya kutoa hapo?

Labda wale ambao tayari wako kwenye mfumo, wakifanya mafekeche kama yale aliyosema Nape na yule DC wa Longido, vinginevyo ni ndoto!
 
Wadada wahitimu wote ambao ajira imewapiga chini nawaombeni sana nendeni kijijini mlikozaliwa mkagombee nafasi za wenyeviti wa vijiji na Halimashauri yake. Sababu Mnazi, uwezo Mano na nia mnayo.
 
Mambo yanayokatisha tamaa ni kwamba jamii zetu Bado Zina watu wengi Ambao Wana umasikini wa mali na akili.
Kama huna pesa jamii haiwezi kukupa fursa ya kuwa kiongozi na suala la kukosa pesa ni changamoto kubwa sio tu Kwa wanawake Bali hata Kwa wanaume Ambao Bado ni vijana na Wana nguvu na akili.
Ndani ya chama Kuna mambo ya rushwa kwahyo kama mwanamke Hana pesa atalazimika kutoa hongo ya mapenzi Kwa baadhi ya watu wenye nguvu ya USHAWISHI ili apate nafasi.

Wanawake nawaoneaga huruma sana kwasababu ili wapate fursa mbalimbali ni lazima watoe rushwa. Karibu 75% au 80% ya wanawake wanaohitaji fursa za uteuzi, ajira, uongozi, elimu n.k hutoa hongo ya mapenzi.
Ndomana Mimi Bado naamini kwamba mke wangu siwezi kumpa ruhusa ya kuomba kazi, uongozi na mambo mengine yani naona ni Bora aendelee kunisaidia majukumu ya nyumbani na kuangalia watoto huku tukiwa tunasubiri kufa.
 
Wanawake wa Tanzania, je, umejipanga kugombea nafasi yoyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu ujao?

Ni sababu zipi zinakuchochea kugombea au zinakuzuia?

Ni kweli Wanawake wanaogopa kujihusisha na Siasa au kugombea nafasi za Uchaguzi?
Hii ni mada maalum ya wanawake kuhusu kugombea nafasi za kisiasa kwenye chaguzi zijazo.. Vema Wababa tukakaa kando tusiwaingilie
 
Hii ni mada maalum ya wanawake kuhusu kugombea nafasi za kisiasa kwenye chaguzi zijazo.. Vema Wababa tukakaa kando tusiwaingilie
No, you are wrong.

Jamii tulizonazo zina mchanganyiko wa Watu wa jinsi zote, Yaani Wanaume na Wanawake na sisi sote tunategemeana katika uwepo wetu hapa duniani. Hakuna jamii ya Wanawake inayoweza ku-exist peke yake bila ya kuwepo kwa Wanaume, na pia Hakuna jamii ya Wanaume inayoweza ku-exist peke yake bila ya kuwepo kwa Wanawake. Hivyo Basi, tunapaswa kushauriana au kutoa mchango wa mawazo kutoka kwa jamii Moja kwenda kwa au dhidi ya jamii nyingine pale inapobidi au inpokuwa muhimu kufanya hivyo.

Wanawake wa Tanzania, je, umejipanga kugombea nafasi yoyote katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu ujao?

Ni sababu zipi zinakuchochea kugombea au zinakuzuia?

Ni kweli Wanawake wanaogopa kujihusisha na Siasa au kugombea nafasi za Uchaguzi?

Mimi siwashauri Sana Wanawake kujihusisha na masuala ya Siasa, hususani Siasa katika vyama vya Siasa, hii ni kutokana na hali halisi ya mifumo ya kufanya Siasa iliyopo hivi Sasa hapa nchini. Siyo siri hata kidogo, Tanzania na Afrika kwa ujumla kuna mifumo mibaya sana ya kufanya Siasa, kamwe hakuna Siasa za kistaarabu hata kidogo, kuna Siasa chafu Sana za maji-taka ya mtaro, na Wanawake wengi zaidi wanaojaribu kuthubutu kuingia huko huwa wanakuwa wahanga wakubwa Sana wa kuchafuliwa Majina yao.
 
Back
Top Bottom