kwa wanawake wenzangu naomba mnijibu swali hili

kwa wanawake wenzangu naomba mnijibu swali hili

Ney maa

Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
95
Reaction score
34
kama m2 umeanza kupata siku zako tarehe moja? siku za kupata mimba ni zipi?:A S 2152:
 
we Tovigale nataka nibebe mimba ntatumiaje condom?
 
Umejiandaje na hiyo mimba?umecheki Afya ya wewe na mwenzi wako?je umemwandalia maisha gani Huyo mtoto mtarajiwa Wa Tanzania hii?
 
Mi sio mwanamke ila naweza kukusaidia kama ifuatavyo
1.Kwanza kabisa inakiwa ujue kuwa kuna aina tatu za mwandamo au mzunguko wa hedhi kwa wanawake moja ni wale wenye mzuko wa wastani yaani siku 28-30 hawa siku zao za ovulation au siku za uzazi(kupata ujauzito ni kuanzia siku 11-18
Mbili ni wale wenye mzunguko mfupi siku 18-24 hawa siku za kupata ujauzito ni kuanzia siku 1-9 hawa ukitaka mtoto inatakiwa ufanye tendo la ndoa akiwa kwenye siku zake mpaka siku ya tisa kuna uwezekana wa kupata mtoto.
Tatu wenye mzunguko mrefu siku 35 au zaidi wakati mwingine mpaka siku 44 hawa siku za uzazi ni kama ifuatayo siku ya 1-4 hapa anakuwa kwenze siku zake tena siku 14-18 halafu tena siku ya 26-30.Hakikisha unaujua mzunguko wako vizuri.
 
Thanks Ngomakipindi wa2 kama nyie ndo nawapenda huku JF wengine kila ki2 wanajibu wanavojiskia 2badilike 2fanye mzaha penye mzaha
 
Umejibiwa vyema, ila ili upate majibu specific ungetaja mzunguko wako ni wa siku ngapi.
Usisahau kumuomba Mungu ili akupe haja ya moyo wako, kwani watoto hutoka kwa Mungu.
 
angalia mzunguko wako niwa siku ngapi,gawanya mara 2 then toa siku mbili nyuma halafu halafu ongeza siku 2 mbele,kuanzia hizo siku 2 za nyuma mpaka hizo 2 za mbele ndio kipindi cha kupata mimba,mfano mzunguko wako ni siku 28,ukigawa kwa 2 unapata 14,ukitoa 2 unapata 12 ukiongeza 2 unapata 16,unatakiwa kuanza kutafuta mtoto tarehe 12 hata tarae 11 kwa maana inategemea mwanaume atakua ametoa mbegu ya ainna gani kama xx au xy,kwa hiyo unaenda mpaka tarehe 16,kwa hiyo angalia mda wa mzunguko wako halafu ufanye hivyo.
 
Thanks Ngomakipindi wa2 kama nyie ndo nawapenda huku JF wengine kila ki2 wanajibu wanavojiskia 2badilike 2fanye mzaha penye mzaha

Haya kila la heri katika kushiriki uumbaji ambao ni Baba,Mama na Mungu.
 
Back
Top Bottom