Huwa nawaza kama mshindi anakuaga ameandaliwa inakuaje sasa mtu kama brock lesnar na hasira zake zote mpk huwa ana loose control akubali kupigwa na mtu kama cm punk! Hapa kwny kupanga mshindi kuna ukakasi, bado siamin km mshindi hupangwa[emoji36]
They are professional trained performers.
Moves zote wanazofanya wanasaidiana ili ionekane ni kweli kitu kinafanyika kwa nguvu sana, ule ulingo si mgumu kama unavyodhani pamoja na kwamba huwa sometimes wanaumia sana lakini wanajua namna gani ya kupigana na watu waone ni kweli jambo linafanyika na kuumizana.
Kwa mfano:
Mtu akirusha ngumi anatakiwa akunje sura ile kuwashilia kuwa anatumia nguvu kuirusha... vile vile anaepigwa anatakiwa aoneshe kuwa nguvu imetumia hivyo kwa pamoja akipigwa ngumi nae anajiangusha au anarudi nyuma kwa kupepesuka kuonesha uhalisia wa jambo.
Pia mtu anaepiga ngumi huwa anapiga miguu chini ili ionekane ni ngumi inatoa kishindo kikubwa kumbe ni miguu ila hii inafanyika kwa pamoja hivyo mtu si rahisi kugundua.
Ulingo umefungwa microphone ambazo zimeunganishwa kwa speaker hivyo mtu akianguka kishindo kinakuwa kikubwa kuonesha impact kubwa ku prove hili ni kwamba hata waangaliaji wote ndani ya ukumbi wakishangilia sauti ya kishindo kutoka ulingoni husikika.
Mshindi anakuwa amepangwa na refarii ndo mwongozaji kuhakikisha hilo linafanyika tena kwa usahihi na muda uliopangwa. N:B huwa mapambano yanapangiwa muda wa kuisha kama dakika 5 , 10 n.k.
Its real intertainment kwamba kinachotokea kinakuwa kimepangwa na jambo linafanyika na watu wakiona.
Wanasaidiana kuhakikisha mtu anaepigwa haumii au akipata maumivu ni kidogo.
Tombstone/ msumari ya undertaker kichwa cha anaepigwa hakibamizwi chini kama unavyoona, mtu anaepiga tombstone anatakiwa ahakikishe kichwa cha anae pigwa kiko juu kidogo ya magoti na anamshikilia kwa nguvu na anae pigwa anamshikilia mgongoni kwa nguvu zote ili asiteleze au kupigizwa chini kweli, kile kishindo kinachotokea kinatokana na magoti ya undertaker kupiga chini kwenye ulingo na si kichwa. Baada ya kupiga tombstone anamuachia kwa kumpeleka mbele ili aangukie mgongo ndo tombstone inakuwa imekamilika.
Chokeslam/ kumnyanyua mtu kwa mkono mmoja na kumpigiza chini ...
Anaenyanyuluwa anajinyanyua ili iweze kufanyika na kumfanya anaenyanyua aonekane ana nguvu nyingi kweli za kumnyanyua mtu kwenda juy kiasi hicho kwa mkono mmoja. Kinachofanyika ni anaenyanyua anamvuta kwa chini kidogo anaenyanyuliwa ili kumuashiria ajianze kujirusha ili wafanye kwa pamoja kunyanyuliwa na yeye kujinyanyua .
Wanamieleka ni wananguvu kweli ila mengine yanafanyika kwa kusaidiana na kurahisishiana.