hapana nilikuwa namuingiza kwenye mtego sasa kuanzia leo nitakuwa nakumbusha kila siku juu ya kumpokea bae wako kutoka jeshiniDaaah!!!! Siamini Macho yangu Mpka APA Nimeamini Kuwa Ata wewe Tegemeo Uko Kwenye Njia Moja Na Huyu Anayetaka kufanya Jaribio La Kuharibu Mahusiano Yangu Na Boo Lee Dahh!!!
Mpaka Apa Nimeamini hii Vita Ulikuwa Unaipika Pika Chini kwa Chini ...na ikifika tarehe 31/10/2017 ningependa uwe wa kwanza kufika kambi ya jeshi kwa ajili ya kumpokea lee seung gi, hivyo basi unapaswa uvunje ratiba ya kuhudhuria harusi ya song couples siku hiyo
hahahaaaaaa lazima aminas akaombe msaada upande wa korea kaskazini akitaka asitake
Hahahaa hii historia yako imenisisimua sana..nimegundua kumbe nilianza kuona Korean drama kabla yako na vingine nilivyogundua siri yangu. However my respect to you will never change maana kutangulia si kufika...nilitangulia mimi kuanza safari ila umenitangulia kufika.ahsante sana na mungu azidi kukubariki pamoja na familia yako yote na sote kwa ujumla.
kama utaniamini mpaka 2013 mwezi kama wa 8 kama sikosei nilikuwa sina uelewa wowote kuhusiana na korean drama, nakumbuka zamani marafiki zangu walikuwa wananihadithia tamthilia kama jumong, queen seondeok wakati zilipokuwa zikionyeshwa kwenye ITV ila mimi nilikuwa wala sina habari nazo kabisa.
ndipo siku moja mama yangu kipenzi alinituma nyumba ya jirani nilipofika kwenye nyumba nikawakuta wanaangalia drama ya jumong tena episode ile ya jumong anataka kuuliwa na bubunno na ndipo nikawa najiuliza.
mbona wamevaa maguo mazito na wanafuga ndevu?
nimehadithiwa jumong ni mzee mbona humu ni kijana?
mbona wanatembea na mapanga ndio maisha gani haya wanayoishi kwenye vijumba vya nyasi?
inawezekana vipi jumong aliyekuwepo zama za zamani akawa hai?
hahahaaaaa nilikuwa mjinga sana
kumbe sikujua kama malaika wa korean drama ananiita kwenye ulimwengu wake
basi siku ya pili nilikwenda kwa rafiki yangu nikamkuta anaangalia drama ya IRIS 1 nikabaki kujiuliza ina maana hawa wakorea nisiowafahamu ni mimi tu?
nikawa najiuliza season ndio nini kwa sababu aliniambia ni season 1 episode 2.
nikafanya mpango nikapata shilingi 1000 kwa ajili ya kununua cd zinazotafsiriwa na nakumbuka jumong ilikuwa ni drama yangu ya kwanza kuiangalia lakini bado nikawa naona kizungu zungu kwa sababu nilikuwa sifahamu chochote kuhusiana na buyeo, han dynasty, goguryeo na mambo mengine ila sikukata tamaa.
kadri nilivyokuwa naangalia ndipo malaika wa korean drama alizidi kuniingiza kwenye utawala wake mpaka nikaanza kufuatilia na sound track na nakumbuka sound track ya kwanza kuipakua ilikuwa ni
dont forget me = baek ji young
baadae nikanunua cd za drama ya IRIS nakumbuka niliiangalia kwa siku 4 na nilivutiwa sana na kim hyun jun (lee byung hun), baadae niliangalia bridal mask, swallow the sun, city hunter, slave hunter, gutale of the fox child, kingdom of the wind na nyenginezo.
ni ngumu sana kuniamini ila sifikishi drama 150 nilizoangalia ila mimi napenda sana kufuatilia story za korean drama kwenye mitandao tokea nimiliki computer.
tokea niwafahamu wakorea
- sijawahi kuangalia movie yoyote ya kihindi nikaimaliza hata kama utanipa million 1 unipe zoezi la kutaja movies za kihindi nitashindwa
- film yangu ya mwanzo na mwisho kuangalia ya kiswahili ni ndoa yangu ya steven kanumba na niliiangalia kwa sababu nilikuwa sijawahi kuangalia film yoyote ya kanumba mpaka anakufa
- sijasikiliza nyimbo ya kizungu zaidi ya mwaka wa 2 na hata ukinipa million 1 nitashindwa kukutajia nyimbo za waimbaji maarufu kama bieber,chris brown,katty perry
- sijawahi kusikiliza na wala kuangalia kipindi chochote cha bongo flavor na kama si jamii forums basi hata taarifa za celebrity kama diamond,ally kiba pamoja na nyimbo zao nisingeweza kuzifahamu
maswali ninayoulizwa mara kwa mara
changamoto ninazokutana nazo
- je unaishi korea : sijawahi kuishi korea na wala sina uwezo wa kwenda korea.
- je unajua kikorea: sijui kuzungumza lugha ya kikorea ila internet ndio inanisaidia kujua maneno ya kikorea na kuyatafsiri pamoja na kupata lyrics za nyimbo
inafikia wakati huwa naona ni bora nisitembelee kwenye thread hii kwani naamini kila ninapotembelea thread hii ndio nazidi kuwa na mzuka wa kufuatilia korean drama ila nashindwa kwa sababu nahisi nitakuwa siwatendei haki hususan pale mtu anapo niquote naona tabu kukaa bila ya kumjibu kwa sababu naogopa atanihisi nina dharau.
- utakuta mtu ananishangaa kufuatilia korean drama lakini yeye anafuatilia bollywood, hollywood lakini hajishangai.
- utakuta mtu ananishangaa kukuta nafuatilia nyimbo za korea na waimbaji lakini yeye hajishangai kwa nini anafuatilia nyimbo za kihindi au za marekani.
tafadhali Khantwe usinicheke nilikuwa mjinga sana ila nashangaa humu munaniona shujaa
hahahaaaaa bora iendelee kuwa ni siri yakoHahahaa hii historia yako imenisisimua sana..nimegundua kumbe nilianza kuona Korean drama kabla yako na vingine nilivyogundua siri yangu
Hahaa nawashwawashwa kama mstaafu sidhani kama nitakaa kimya mpaka keshohahahaaaaa bora iendelee kuwa ni siri yako
Siangalii ng'oo...wewe na hao ndugu zako mmeshanifanya mjingaSBS(seoul broadcasting station) imemtangaza muigizaji yoon kyun sang na jung hye seong kuwa waigizaji wakuu wa drama mpya inayotarajiwa kuonyeshwa siku ya jumatatu na jumanne inayoitwa DOUBTFUL VICTORY.
kama Yoon Kyun-sang atakubali ofa hii atacheza uhusika wa Oh Il-Seung ambaye ni askari mdanganyifu (fake detective) ambaye alikuwa anapambana na watu waovu na kumshinda monster na itakuwa ni drama yake ya pili kuigiza kama muigizaji mkuu baada ya rebel thief who stole the people (hong gil dong)
mwanadada Jung Hye-seong atacheza uhusika wa askari anayejulikana kwa jina la Jung Hye-seong.
kwa mujibu wa label ya Popeye Entertainment ambayo inamsimamia Yoon Kyun sang wanasema ya kwamba yoon amepokea ofa mbili mpaka sasa na ofa moja ni kutoka kituo cha televisheni cha KBS2 ambapo nako amepewa ofa ya kuwa muigizaji mkuu wa drama inayoitwa Jugglers ambayo nayo itaoneshwa siku ya jumatatu na jumanne kwenye mwezi wa december hivyo basi drama zote mbili zitakuwa na ushindani hivyo basi tunapaswa kuwa makini kuchagua ofa ilio sahihi.
kama Jung Hye-seong atakubali ofa hii basi itakuwa ni kazi yake ya kwanza kuigiza kama muigizaji mkuu wa kike ambapo kwa sasa anashiriki kwenye drama inayoendelea kwenye kituo cha KBS 2 inayoitwa MANHOLE : FEEL SO GOOD
Hahahaa hii historia yako imenisisimua sana..nimegundua kumbe nilianza kuona Korean drama kabla yako na vingine nilivyogundua siri yangu. However my respect to you will never change maana kutangulia si kufika...nilitangulia mimi kuanza safari ila umenitangulia kufika.
Mimi Korean drama ya kwanza ilikuwa Jumong mwaka 2010...kipindi hicho nilikuwa part timer kwenye ofisi moja hivi basi kuna staff mmoja akawa anakuja na CD za Jumong nikawa naangalia nikipata nafasi basi nikajikuta nimeshaanza kuipenda nikaanza kuifuatilia (cha ajabu sijawahi kuimaliza wala mwanzo wake sijui ulikuwaje). Baadae katika kupitapita kwake nikakuta anaangalia nyingine ambayo sikufanikiwa kujua jina lake.
Nilipoondoka hapo nikawa nimezisahau...siku moja nikiwa chuo nimeenda stationery kuprint assignment (2013) nikaona yule kaka anaangalia A man called God nikaichukua ...kwanza nikashangaa kuona kumbe na hizi za kuvaa suti wanacheza, maana yule kaka alikuwa anaangalia historical tu. Nilipoimaliza nikaenda kuchukua Innocent Man kuanzia hapo ndo ugonjwa wangu ulipoanzia ingawa sikuwa naweza kudownload hata kwa watu wengine ilikuwa sio rahisi kuzipata kwa hiyo nilikuwa naangalia kwa kubahatisha. Kwa mwendo huohuo nikaangalia Emperor of the Sea na rafiki yangu akagundua ugonjwa wangu akaniletea City Hunter. Baada ya hapo ndo nikaanza kuzisaka kwa watu baade nilipogundua kudownload full raha japo bado nachukua kwa watu na ndio hapo nilipoanza kufuatilia Korean drama beyond screen. Katika maisha yangu yote niliwahi kununua CD moja tu ya Emperor of the Sea.
Hebu kila mtu anayejisikia ashee story yake jamani[emoji13] [emoji13] kama hamtojali lakini
hahahahaaaa bado namtafuta yule aliyesema ameangalia korean drama zoteSiangalii ng'oo...wewe na hao ndugu zako mmeshanifanya mjinga
Mimi kdrama ya kwanza kuiangalia ilikuwa ni iris kipindi hicho nilikuwa member wa kudumu wa bolywood na nilikuwa najua Bollywood mpaka nakera katika iris pia nilipenda sana story ile na ost ilopigwa kipindi starling wa iris anakufa kama sikosei kwa ajali ya gari na yule msichana yukk ghorofan na mimba yake.........ilipita miaka mpaka mwaka wa Jana baada ya kumaliza six nikawa naenda kwenye library ya CD kwa jirani hapo sasa ndipo nilipokuta wanaangalia monster ile ya kina kang ki tan na byun lee jae basi kesho niliporudi kwenye library hiyo wakaniambia wao wameshaangalia so bora tuendelee wote dah nikasema hapana nakumbuka usiku huo nilipambana sana ndipo nikaja kuangukia kwenye application ya viki basi safar yangu ikaanzia hapo........kwa wiki naangalia full korean drama zipatazo nne
- hahahahaaaa kipindi unaanza kuangalia korean drama mimi nilikuwa nalala saa 3
- nilikuwa nikiingia kwenye internet naangalia habari za mpira tu.
- nilikuwa siangaliii televisheni
Malizia kabisa sema nilikuwa darasa la tano B
- hahahahaaaa kipindi unaanza kuangalia korean drama mimi nilikuwa nalala saa 3
- nilikuwa nikiingia kwenye internet naangalia habari za mpira tu.
- nilikuwa siangaliii televisheni
[emoji23] [emoji23] [emoji23] haiwezekani hiyo kitu wewe. Labda aseme hasomi, hafanyi kazi, ana mtu wa kumhudumia yaani anampikia anamletea kuimaliza kula anakuja kutoa vyombo, anafua, anapasi na mausafi yote anafanya yaani kazi pekee anayofanya ni kuoga na kula. Asilimia kubwa watu Korean drama tumezijulia kwa Jumong na zilizochezwa kabla ya hapo ameona zote?hahahahaaaa bado namtafuta yule aliyesema ameangalia korean drama zote
Aisee hiyo black hiyoo[emoji13] [emoji13] lazima niionekorean drama zitakazoanza wiki hii
- 20th Century Boy and Girl
Time slot: Monday & Tuesday
Broadcaster: MBC
Genre: Romantic comedy
Episode count: 32 (half-hour episodes, 16 hours in total)
- Witch’s Courtroom
Time slot: Monday & Tuesday
Broadcaster: KBS
Genre: Legal drama
Episode count: 16
- Because This Life Is Our First
Time slot: Monday & Tuesday
Broadcaster: tvN
Genre: Cohabitation romantic comedy
Episode count: 16
- Mad Dog
Time slot: Wednesday & Thursday
Broadcaster: KBS
Genre: Crime thriller
Episode count: 16
- Go Back Spouses
Time slot: Friday & Saturday
Broadcaster: KBS
Genre: Time-travel romantic comedy
Episode count: 16
- Black
Time slot: Saturday & Sunday
Broadcaster: OCN
Genre: Supernatural thriller
Episode count: 16
- Revolutionary Love
Time slot: Saturday & Sunday
Broadcaster: tvN
Genre: Romantic comedy
Episode count: 16
Wewe. NNE? Aisee mimi ni mlevi ila we nahisi tejaMimi kdrama ya kwanza kuiangalia ilikuwa ni iris kipindi hicho nilikuwa member wa kudumu wa bolywood na nilikuwa najua Bollywood mpaka nakera katika iris pia nilipenda sana story ile na ost ilopigwa kipindi starling wa iris anakufa kama sikosei kwa ajali ya gari na yule msichana yukk ghorofan na mimba yake.........ilipita miaka mpaka mwaka wa Jana baada ya kumaliza six nikawa naenda kwenye library ya CD kwa jirani hapo sasa ndipo nilipokuta wanaangalia monster ile ya kina kang ki tan na byun lee jae basi kesho niliporudi kwenye library hiyo wakaniambia wao wameshaangalia so bora tuendelee wote dah nikasema hapana nakumbuka usiku huo nilipambana sana ndipo nikaja kuangukia kwenye application ya viki basi safar yangu ikaanzia hapo........kwa wiki naangalia full korean drama zipatazo nne
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]nakumbuka rebel niliangalia Siku 3Wewe. NNE? Aisee mimi ni mlevi ila we nahisi teja