mjr95 nimeanza kukuogopa kwa haya maandishi yako mawili ya mwisho ndani ya thread hii na itanibidi nikuite sunbae, tafadhali sana
EMPTY dongsaeng usiniite tena sunbae kwa sababu anayestahili heshima hii ameshajidhihirisha baada ya kujificha kwenye mchicha kwa muda mrefu akidhania hatojulikana.
without discipline, order will crumble. And without order we can't fight the enemy. I would do worse to stop the order from crumbling
maneno hayo nakumbuka aliyazungumza kwenye episode ya tatu baada ya wanajeshi watatu kuamua kujaribu kukimbia kambini na ndipo akatoa amri ngumu sana ya kuuliwa na vichwa vyao kuwekwa katikati ya mji ili iwe fundisho kwa yeyote yule atakayejaribu kwenda kinyume na amri ya jeshi la majini haijalishi anayevunja amri ana cheo kiasi gani.
kwenye andiko lako umemaliza kila kitu kinachomuhusu mwanadamu huyu anayejulikana kwa jina la yi sun shin ambaye takribani vita vingi alivyopambana alikuwa na upungufu wa wanajeshi na hata huduma muhimu kama chakula,usafiri na hata dhana za kisasa za kupambana na maadui.
jaribu kufikiria joseon walikuwa wanategemea zaidi mishale na majambia wakati wajapan walikuwa na ubongo wa mzungu (bunduki) lakini bado japan aliambulia kipigo chenye kuumiza kutoka kwa yi soon shin, unajua kwa nini japan walikuwa wanashindwa na joseon?
sababu ni ndogo tu wajoseon walikuwa na mwanadamu mwenye ubongo hatari zaidi ya bunduki, wahenga wanasema ni bora unyimwe mali kuliko kunyimwa maarifa.
mjr95 nitakapofikia episode ya 10 ya hii drama nategemea kuiweka kiporo kwanza ili niivutie kasi ya kuja kuiendeleza tena.
sisi sote ni wanajeshi wenye dhambi kubwa sana ya kuwaua maelfu ya ndugu zetu ndani ya bahari hii kwa miaka 7,kama tutashindwa kuimaliza vita hii kwa ushindi basi tutakuwa tumeshindwa kurudisha furaha na amani ya wanachi wa joseon na pia tutakuwa tumeshindwa kuwafanya marehemu kupumzika kwa amani huko waliko na dhambi zetu zitaendelea kubakia, leo hii wanajeshi 16000 tunakwenda vitani huku sura zetu na nafsi zetu zina dhambi lakini kesho tutarudi huku sura zetu zikiwa na furaha ya ushindi,katu tusiache hata meli moja na mwanajeshi mmoja wa kijapani kurudi kwao akiwa mzima wa afya.
lakini maisha yote wanasiasa ndio watengenezaji na waharibifu wa nchi jaribu kufikiria jinsi gani mfalme seonjo alivyokuwa na bifu na mtumishi wake kisa ni kwamba yi soon shin anapendwa sana na watu kuliko yeye, ndio maana mimi
Damushin siipendi sana siasa wala jukwaa la siasa.
duh! huku kwetu vilipotokezea vita vya kagera baadhi ya wazee niliwahi kuwasikia wakijisifia eti walikula sabuni ili wapate ugonjwa wa kuharisha na wasichaguliwe kwenda vitani, hahhahahhhahahahhhahaha chezea uhai.pumbavuuuuuuuu