Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

kuna hii KILL IT NITAIPATA WAPI maana mimi na muvi za kipelelezi damu damu



Donwload hiyo app mkuu, utaikuta na nyingine nyingi za kijanja...!!!!!
 
Hongera kwa msiba? [emoji22][emoji22][emoji22] sunbae
ahsante sana, sisi wengine bila ya kufa kwa binadamu hatupati fedha ya kuendeshea maisha yetu.
wachimba makaburi na wachongaji majeneza oyeee.
mashekhe na maaskofu ambao kazi zetu kubwa ni kusalia maiti oyeeee.
nyakati za ibada waumini wanatukimbia lakini nyakati za kusalia marehemu kijacho lazima waje kwenye nyumba ya ibada tuwarambe fungu la 300
 
[emoji3][emoji3] aisee
 
umeshatayarisha nguo nyeusi?
au msiba wa tajiri sisi malofa haturuhusiwi kula ubwabwa?
shida yangu kula tu wala sina habari na ubuyu wa marehemu
[emoji3][emoji3][emoji3] hayo ndio maneno, hivi unakulaga ubwabwa? Najua unakulaga tu kimchi, ramen, noodles e.t c
 
[emoji3][emoji3][emoji3] umeanza mambo yako
 
Niombe radhi kwa lugha yetu
naomba radhi kwa tabia yangu mbaya nilioinyesha kwako, nafahamu umeshanikataza zaidi ya mara tatu niachane na utani wa neno jasusi lakini nimeshindwa kufanya hivyo.

nafahamu kuomba kwangu radhi hakutabadilisha tendo lililokwisha pita hapo nyuma lakini kuomba kwangu radhi ndio njia moja muhimu itakayoniwezesha kutengeneza mahusiano bora hapo mbeleni.

kwa sasa ukurasa wetu wa mahusiano yetu kama marafiki umevamiwa na hackers kiasi ambacho taarifa zetu zinashindwa kupatikana mtandaoni. je unaweza kuniruhusu kubonyeza kitufe cha refresh ili niweze kurudisha tena mahusiano yetu ya kirafiki kati yetu?
mianhaeyo = 미안해요
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] haki nimecheka ujue wewe sio mzima
 
Daah! Unaambiwa kwenye kaburi la General Choi Young, Majani yaliota kwa mara ya kwanza 1972, since alipokufa mwaka 1388, hata hivyo yeye ndiye aliyetamka majani yasiote katika kaburi lake kama ishara ya uovu aliyoufanya, pamoja na hayo General Choi Young ni mtu anayeheshimika mpaka leo na anachukuliwa kama mfano bora mpaka sasa.
Jambo la kufurahisha hata drama ya Jeong Do-Jeon imeeleza kama ilivyo andikwa kwenye history.
 

Lee Yo Won wangu jamani nimemmiss, nangoja isogee sogee kidogo nianze kuicheki na mimi.
 
thanks mkuu
tumeletwa dunia kwa dhumuni la kutenda mema, kudumisha urafiki wetu wa kibinadamu
bila ya kusahau tumeletwa dunia kwa dhumuni la kusaidiana pindi mmoja wetu anapokuwa na shida haijalishi ni ndogo zaidi ya chembe ya mchanga.

karibu tena kijiweni kwetu moja kati ya sehemu isiyobagua jinsia ya mtu, kipato cha mtu, rangi ya mtu haijalishi ni kijani zaidi ya bendera ya chama tawala.
jisikie huru kutembelea hapa na pia ujisikie huru kuondoka hapa huku ukituachia furaha kwa njia ya comment.​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…