Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Series gani Kali ya mdawote?
Nimeliona neno 'ya' hapo kwenye swali lako na kutokana na hilo neno nafikiri unahitaji kutajiwa au kupewa jina la Project 'Moja' tu ambayo ipo juu (juu zaidi) kuliko nyingine zote katika ulimwengu wa Series hususan 'Drama' za Kikorea.

Hilo swali (tukiacha utani) ni gumu sana kulijibu na liko 'Very Limited' ila pamoja na hayo nitajitahidi kulijibu kama ifuatavyo;

Katika utafiti wangu nilioufanya nikizingatia pia vigezo na mawazo ya watazamaji wengine na pia bila kusahau mitazamo ya wadau kutoka vyanzo mbalimbali, nadhani hii hapa chini inaweza kuwa jibu la swali lako;
  • Jewel In The Palace

Sababu zipo nyingi sana kuitaja hiyo 'Drama' hapo juu ikiwemo jinsi gani ilivyoweza kujizolea umaarufu mkubwa Duniani Waingereza wanakuambia; International Hit, Drama ambayo imerushwa na vituo mbalimbali vya runinga zaidi ya nchi 90 Duniani. Si mchezo!

Pia hiyo 'Drama' ni moja ya chanzo kikubwa cha 'Utamaduni' wa Kikorea kuenea nchi mbalimbali Ulimwenguni bila kusahau pia nchi moja 'maarufu sana' inayofahamika kama 'Dona Kantre' iliyopo kule Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Nadhani nimekujibu swali lako.
 
Ina episode ngapi boss
 
habari waheshimiwa Mimi natumia simu kudownload series za kikorea na tumia app ya dramania ila siku hizi haukubal kudownload episodes tatizo ni nini et?
 
Naona imeharibika jaribu hapa daebakdrama.com
habari waheshimiwa Mimi natumia simu kudownload series za kikorea na tumia app ya dramania ila siku hizi haukubal kudownload episodes tatizo ni nini et?
Baba Swalehe

Unaweza pia kutumia daebakdrama.com unaingilia Google then ukishaingia unakutana na drama kibao unadownload unayoitaka
 
Kimya chenu kinanikera, ina maana kuna mtu mwenye assignments ngumu kuliko miye?!
Episode 200 + Episode 158
Lakini bado nahudhuria humu.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Mimi nipo na Empress Ki sehemu ya tisa si unajua mimi ni mtu wa nyuma nyuma sana mpaka nyie msifie kwanza ndo mimi nafuatilia baadae
Kwa hiyo usijali mkuu tupo pamoja japo na mimi nakereka pia kwa ukimya huu
 
Kimya chenu kinanikera, ina maana kuna mtu mwenye assignments ngumu kuliko miye?!
Episode 200 + Episode 158
Lakini bado nahudhuria humu.
'Ubize' nao umekuwa mwingi kiasi cha kuwafanya wadau waonekane kama wamepotea kambini na huenda wakarejea kundini pale 'ubize' utakapopungua.

Wengine pia huenda wamejipa 'likizo' kutokana na baadhi ya Projects walizokuwa wakizifuatilia kusimama kwa muda na huenda wakarudi kundini pale Projects hizo zitakaporejea hewani.

Kimya kingi kina mshindo mkuu!
 
Haaha Upo huko ndani na Kina mdada yule( Lady Ki) alikuwa jeuri sana.
 
Kweli kabisa, ubize katika masula mbali mbali una chagiza.
Ila tusiruhusu, ubize ukawa chanzo cha kudhohofisha mahusiano yetu, kila kitu kinaongozwa na akili, katika ulimwengu huu wa nyama. Tusiruhusu matukio yatuongoze.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…