Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

VAGABOND Hii Kitu, Korean Entertainment Ahsante. Stori Tamu Inasisimua Kila Scene Haipiti Bure,
Ina Mtiririko Mzuri Hakuna Nguo Za Ndani Wazi Mule Ndani Wala Mwili Wazi, Hakuna Viungo Vya Wakike Wazi Mule Ndani Na Bado Inakufanya Uhitaji Kuingilia Kila Inapotoka.

Wametengeneza Kitu Kiutamaduni Wao Na Bado Kinavutia.

Tanzania Yangu Tunakosea Wapi!?!
 
Yes Vagabond Ni real deal
Graceful family ilikua inaenda vizuri Mara naona wanaikimbiza kimbiza kuisha
My country....am shipping with this too
Jaman ya katikat ya wiki drama nzuri Ni ipi, maana kusubir kulipukwa moyo weekends tu Sion Raha

Alafu huko telegram Mimi kwangu havidownlodiki bundle la usiku alaf inazunguuka sana
 
Share link ya telegram basi mkuu
 
Tale of Nokdu Nayo Si Mbaya
Ndo Drama Za Kati Ya Wiki Ninayoangalia
 
Yea exactly. Yaani kila episode mwili unakusisimka.
 
Mmekuwa wakimya si tu humu hata kule Telegram
channel ile inawahusu watu wote waliojiunga ukiwemo wewe muhuni kutoka usukumani ndio maana muanzilishi alizungumza hivi ndani ya thread hii.

'' kama kuna yeyote atakaye hitaji kushare movies au drama za kikorea basi anitafute private ili nimpe ufunguo wa kuingia ndani ya channel ili apate kuapload hizo project zake alizonazo.''

wala hakuandika hivi:

'' siruhusa kwa member yeyote kuapload videos au picha kwenye channel hii isipokuwa Nifah na daemusin.''


====================================
Tanzania haiwezi kujengwa na magufuli peke yake, hivyo basi ni wajibu wa kila raia mwenye akili na asiyekuwa na utimamu wa akili kujitolea kwa jasho lake kuipigania nchi hii inayoongozwa kwa misingi ya kidemokrasia inayoruhusu kuwepo kwaa uhuru wa kusifu na kukosoa kwa nidhamu na staha ile ya kibinadamu pale zuri au ovu linapotendeka na si kuongozwa na umajinuni wa kukejeli au kudhihaki pande hasimu kwa pupa kama mnyama mwenye ashki zisizoepukika.

hata ile channel nayo haiwezi kusonga mbele kwa kumtegemea muanzilishi wake au huyu mjinga anayeitumia username ya daemusin humu ndani.


=====================================
daemusin bin vipigo kwa mashangazi zenu wa mtwara na lindi si nabii na hatokuwa nabii aliyeletwa kuwakomboa wana waizraili waliopotezwa na upepo wa bongo movies, nigeria, india na american ili waitafute njia sahihi ya kuelekea KOREA.

'' haitokuwa sahihi kutumia nguvu kubwa au ndogo ya ummah kwa lengo la kuugeuza wema uliotendwa na kundi fulani uonekane kama ni utumwa kwa wengineo wanaojificha kwenye mwamvuli wa ubwanyenye na ubepari wa kutenda wema huo huo

kuepusha hilo ni wajibu wetu sote kwa pamoja kuongozwa zaidi na ikhlasi inayoambatana na ihsani kutoka nafsini mwetu ya kulitenda jambo hili kwa pamoja kwa mukhtadha wa kulifikia lengo lilolikusudiwa bila ya kuwaza ni kiasi gani cha muda na mali utakaopotea''

kuendelea kuutegemea muhimili mmoja utekeleze operations zote muhimu zinazotuhusu ndio mwanzo wa kuukaribisha udikteta wa maneno yasiokuwa na busara mbele ya hadhira na baadae kufuata udikteta wa matendo yatakayoumiza pande zote zinazofurahia na zisizofurahia uparasite wa fikra na matendo.

  • kabla yangu mimi hakuna aliyewahi kutenda haya.
  • hivi nikiondoka mimi atakayekuja atayatenda haya niyatendayo?
  • nisipofanya hili nitafanywa nini na wengineo haliyakuwa mimi ndiye muhimili muhimu zaidi?
  • acha leo niwakomoe kwa kutokupost chochote au kutenda lolote
  • acha leo niwatukane hadharani kwa kuendelea kunitegemea mimi kama muhimili.
  • acha niwakimbie hawa parasite wasiojielewa
kuna njia moja tu ya kuyaepusha hayo yasitokezee, kila mmoja anapaswa kutimiza wajibu wake.
tutafanya makosa makubwa sana kama tutalizalisha tabaka litakalojiona muhimu zaidi ya wengine na hapo ndipo tutakapomzaa mobutu seseko wa channel ile na nchi ileeee ilionunua kunguru waroho wa operating cost na production cost watakaopelekea kuzalishwa kwa lose au break even kwa sababu ya kukosekana mshauri sahihi kwa bwana yulee.
======================================

karibu pyongyang
wang guhn anasemaje hukooo na wake zake 30?
ryu seong ryeong anasemaje hukoo na kitabu chake cha jing birok?


NB:
weweee bwegee kutoka usukumani munakokula mihogo ya kuchoma kwa ndimu kama panya usije ukadhani nimechukizwa na comment yako hapo juu niliyoinukuu.
korean drama forever
 
Kuna mpuuzi Fulani toka Pyeongyang mwenye fikra finyu kama maisha ya Kinyonga mjamzito aliwahi kusema" Collaborative thoughts bring success"
Bilashaka huyo mjinga anakubaliana na yote uliyozungumza.
Sasa miye ni nani mpaka nipate uthubutu wa kupinga ukweli?
Samahani sana dada ( Nifah ) huu ujinga wangu umenifanya kipofu looh! Najisikitia mwenyewe, looh! Juzi nilikuwa na drama ya God of War( Soldier) 1-30. Kwa ujinga niliyokuwanao nikashindwa kukumbuka kulee, kwa bahati mbaya nishaifuta.haitokuwa busara kuleta kichwa kisicho na kiwiliwili.

Narudi kwako Daemusin mtu akishajua kuwa yupo gizani jua kuwa tayari ashaanza kuona mwanga. Kwahiyo ujinga wangu unaanza kutoweka.
 
upcoming drama: VIP
Release Date:
October 28, 2019 (kesho)
Runtime: Monday & Tuesday
Episodes: 16

Na Jung-Sun (Jang Na-Ra) works for a team that deals with VIP customers of a department store. She is married to Park Sung-Joon (Lee Sang-Yoon), who works on the same team. The couple faces an unexpected case, which causes their lives to fall apart.

dondoo fupi kupitia press conference iliofanyika siku mbili zilizopita​

PD (producing director) Lee Jung Rim amezungumza kwa ufupi :
ni stori inayojaribu kuangaza maisha ya kila siku wanayoyapitia wanandoa ikiwemo furaha, huzuni, dhiki yanaunganishwa na siri zilizofichwa ndani ya nafsi zao. kuna mambo mengi ya kushangaza mutakayoyashuhudia kwa kila episode ya drama hii. Kwa mara ya kwanza muandishi alipokuwa akifanya uchunguzi wake alishindwa au hakufikiria kudesign timu itakayohusika kuwahudumia wateja maalumu (VIP), mara nyingi tumezoea kushuhudia marketing team ndiyo inayohusika na shughuli zote za kuuza au kuwahudumia wateja, lakini kiupande wetu tuliona itakuwa ni jambo zuri zaidi kiubunifu kama tutaswitch (kubadilika kifikra) kutoka marketing team hadi kutengeneza department store itakayohusika na utoaji huduma kwa wateja maalumu (VIP).


Jang Nara
mahusiano yake ya ndoa pamoja na mume wake yalianza kubadilika baada ya kupokea ujumbe wa kushangaza na kutia khofu ndani yake unaomuhusu mume wake. Tulipokuwa tunaigiza hii drama haijawahi kutokezea hata mara moja muigizaji mwenzangu ambaye ni Lee Sang Yoon kunifanyia jambo lolote baya ambalo lingenipelekea nisijisikie kuwa na furaha na amani ndani ya kiwiliwili changu (uncomfortable). Nimeamua kushiirki ndani ya drama hii kwa lengo la kuonyesha pande zote mbili kwa usahihi zinazomuhusu na jung sun.

Lee Sang Yoon

baada ya kukaa sote kwa pamoja waigizaji na kujadili the acting style (sijapata neno sahihi la kiswahili) itakayotumika kupitia drama hii nimegundua mambo mengi sana yenye kufanana kati yetu, ni jambo la faraja sana kufanya kazi na kundi la watu munaoelewana kimtazamo.


baada ya miezi takribani minne kupita hatimaye kituo cha SBS wanarudisha tena drama kwa siku ya jumatatu na jumanne.

nina miezi miwili na nusu sijaangalia drama za jumatatu na jumanne hivyo basi huenda hii ikanirudisha tena kwenye ulimwengu wa blue monday,
jang nara pamoja na lee sang yoon ni waigizaji wenye nguvu sana kwenye huu ulimwengu wa sanaa nchini korea ila nguvu pekee ya muigizaji bila ya kuwepo mazingira bora ya kikazi yanayoambatana na good scripting hayawezi kuifanya drama iwe na mafanikio hata kwa njia ya miujiza.

Natumai stori yake itakuwa ni moto zaidi ya mgahawa wa camellia a.k.a dongbaek

 

Attachments

  • 1572181643211.png
    348.2 KB · Views: 3
"karibu pyongyang
wang guhn anasemaje hukooo na wake zake 30?
ryu seong ryeong anasemaje hukoo na kitabu chake cha jing birok?"



Msimulizi wa Drama amesema kwamba Ile drama Imeruka story ya WANG GEON na wake zake. WANG GEON anajenga Palace kule Pyeongyang kama Ishara ya Kumuenzi King Gwanggaeto na Gogryeo yake, na wana ndoto ambazo hawatokuja kuzimiza( Ndoto ya kuifanya Goryeo iwe na Eneo kubwa Kama la Gogryeo hasa kuelekea Magh na Kas).

Kule Kyeon Hyeon anaishambulia Shilla( λŒ€μ•Ό μ •/ Daeya Fort) kwa mara ya tatu. Nina Imani Round hii muhuni atashinda


Ryu Seong Ryeong, Gwanghae na watumishi wengine, hawamuelewi Seonjo hasa kwa tabia ya yake ya ubinafsi.
Mbali na hayo kiukweli Huyu Gwanghae ni moja kati ya watu ambao wanapaswa kuja kukumbukwa sana. Najaribu kufikiria kama akishika kiti cha enzi, atakuwa na Wakati mgumu mno, maana Vita vitakuwa vimeacha Athari nyingi sana, changanya na Wanasiasa ambao wanajali tu, kupata ama kuongeza nguvu za kisiasa, na si kuungana katika kipindi hicho kigumu. Nawaza tu Huyu Gwanghae ukiwa na watu 10 kwenye Baraza lako kama Ryu Seong Ryeong tumaini lazima liwepo si tu serikalini mpaka kwa Watu.
Mi naamini Ryu Seong Ryeong Alikuwa na mahaba na Taifa lake. Pia nimejifunza kuwa mzalendo anawaza juu ya maendeleo ya Taifa lake na kujenga misingi bora kwa Kizazi kijacho while Wanasiasa wanawaza namna ya Kuongeza Ushawishi na nguvu za kisiasa.
Laiti kama Mfalme Seonjo angemsikiliza jamaa( Ryu Seong Ryeong) wala Maradhara makibwa yasingetokea.
HADHINA YA TAIFA.
 
Kha!!! Hii drama ya god of War ni tamu kila Episode loh![emoji16][emoji16]
Wacha niendelee kupata uhondo mie.



[emoji16] Mmekuwa wakimya si tu humu hata kule Telegram
Hiyo seasoni ni kali we acha tu sijui kama kuna season ya kuushika huo moto.
 
Nahitaji mnitajie season kali kuzidi six flying dragon
Mzitoe
Greet queen, empress ki na flower in prison.
 
Hiyo seasoni ni kali we acha tu sijui kama kuna season ya kuushika huo moto.
Napoiona Hii drama na ninapomtazama KIM JUN naona kama mizimu ya KING GWANGGAETO THE GREAT ( DAM DEOK) imemuingia ndani yake, yaani anageuka mnyama Dam deok anapopigana, KIUKWELI DRAMA ZA KIBABE KAMA HIZI NA STERLING ANAPOKUWA NA MIZUKA KAMA HII NACHEKEA MOYONI.
 
daebak, muda huu ndio nimemaliza kuingalia hii drama episode mbili za wiki hii (mpira wa ulaya nimeusamehe kwa siku ya leo). zimebaki episode 4 ili hii drama imalizike na sijajua kama kutakuwepo na uwezekano wa seson 2 japokuwa ningelipenda uwepo muendelezo wake kwa sababu nahisi stori ndio kwanza inachangamka, binafsi nimezoea episode 16 zenye kubeba wastani wa dakika 70 - 90 kupitia tvN tofauti na hiki kituko wanachotufanyia SBS cha kutuonuyesha lisali moja lilisilotimia kwa kila episode kana kwamba hii drama imebeba episode 20.

jessica lee ni mwanadada ambaye ana uwezo wa kusurvive kwenye hali yoyote ya hatari haijalishi anapambana na simba akiwa peke yake ndani ya chumba kisichokuwa na mlango, harakati zake kama lobbyist za kuhakikisha kampuni yake inajiweka ukaribu na wenye nguvu kubwa za kuwaongoza walalahoi zinanikumbusha drama ya lobbyist ambapo alikuwemo mwanadada lobbyist anayekwenda kwa jina la Maria ambaye na yeye hakuona tabu kuutumia mwili wake kama chambo kwa lengo la kuu la kumteka mteja wake kifikra na kimaamuzi.

Ameshinda dili la kusupply ndege za kijeshi lakini bado anainyemelea tenda ya mafuta ambayo waziri mkuu amemwambia raisi tayari anaye partner hivyo basi haitokuwa jambo rahisi kumuingiza jessica lee kwenye project ya mafuta.

je huyo partner aliyemlenga waziri mkuu ni nani?
nina wasiwasi huenda partner akawa ni Edward Park na kampuni yake ya dynamic ambayo pia ni kampuni pinzani, hivyo basi kuna uwezekano waziri mkuu naye ana upande wake anaoshirikiana nao kama ilivyo kwa bwana Yun aliyejiweka karibu na jessica.

halafu kuna issue ya slush fund: hii serikali yote hakuna aliyemsafi kuanzia raisi mwenyewe hadi muajiriwa anayesafisha choo cha raisi wote ni baba mmoja na mma mmoja. Nje ya drama serikali kama hizi zimejaa zaidi ndani ya bara letu la afrika ndio maana vita ya ufisadi na uwajibikaji inaendelea kuwa ni ngumu haijalishi teknolojia ya sasa imepevuka na sababu kubwa ni kukosekana kwa uwazi hususani juu ya matumizi ya serikali, mara nyingi mafisadi na madikteta hujificha kwenye mwamvuli wa kuwapambania wananchi ili wapate stahiki zao na wakati huo huo kwenye nafsi zao wakiongozwa zaidi na ubaya wa kutamani kupora kila kilicho mbele yao.

inaonekana dhahiri secretary Yun ndiye engine kuu ya muheshimiwa raisi kwenye mission zote chafu zinazomuhusu muheshimiwa aliyejificha kwenye kivuli cha utakatifu, kinachokwenda kutokezea baadae ni watatu hao kusalitiana hapo mbeleni kama itatokezea kuvuja kwa siri ya kuwepo kwa mlolongo wa rushwa kwenye dili la kununua ndege za kivita.

mpaka sasa mtu pekee mwenye uhakika wa kusurvive kwenye hili pambano licha ya kuwa naye ni mchafu wa matendo na si mwengine ni waziri mkuu kwa sababu ana ushahidi mwingi sana unaomuhusu muheshimiwa raisi pamoja na waziri wa ulinzi (tukumbuke mwanzoni drama waziri wa ulinzi alihongwa rushwa tofauti na bi jessica ikiwemo rushwa ya ngono na picha zilimfikia muheshimiwa raisi)

heshima kwake bwana judge kwa kuchelewesha kesi licha ya kupokea oda ya kuimaliza kesi ile kutoka chief justice ambaye alikwisha pokea amri kutoka kwa muhimili mchafu (jessica na crew yake)

kama raisi ndiye bingwa wa kupokea rushwa kutoka kwa matajiri unadhani rushwa hii itaweza kuondoshwa kwa mikono yake hususani kwa kuwatishia vyanzo hivi vya chini vya utumishi vinavyoendelea kupokea mshahara wa chini baada ya makato na kodi?

rushwa haiwezi kuondolewa kwa rushwa.
ufisadi hauwezi kuondolewa na mfumo fisadi.
ni sawa na mtengenezaji pombe kuweka tangazo la kukataza ummah uliopotea kunywa pombe.


dah! kadri ninavyomuona my love from joseon hwang bo ra moyo wangu unakatika vipande vipande kama samaki. Wengine wanajileta kwangu nakuniambia kwa nini usinipende mimi daemusin matokeo yake nabaki kuwajibu.


kama wewe kama wewe upendwe nini ?
siwaumbo si wa nywele si wa ghuyuni,
mbele zero nyuma hakujulikani
baraka ya wanja, kujipakaza machoni
kwenye visura wewe huko hisabuni
Zunguka bongo waone kila mahala
figure zao za kupigiwa mfano
sio zumbukuku na shepu ya penseli
hivyo unadhani kwa yakini watakiwa kwa uzuri gani hasa wa kujizuzua

sibasi tu sibasi tu sibasi tu




next: my country drama ndipo nilale.
sitaki niamke kesho nikiwa na fikra za kuangalia korean drama haijalishi ni kwa nusu saa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…