Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Vyanzo vingi vya kihistoria vinakielezea kifo cha Bidam nyakati ambazo Queen Seondeok alikwisha kufa, mapema sana wakati uasi unaanza rasmi.

Na baada ya kifo cha Seondeok, kiti cha Ufalme kilichukuliwa na binamu yake ambaye ndiye huyo Jindeok ambaye alikipokea kijiti na kuendeleza mapambano dhidi ya waasi (akina Bidam) mpaka pale uasi huo ulipofutiliwa mbali.

Kwa maana hiyo nadhani, King's Dream Drama imefuata mtiririko huo tofauti na Queen Seondeok Drama ingawa kwa upande wangu Queen Seondeok Drama inasimama vizuri zaidi.

Pia, waandaaji wa Projects husika huwa wanajaribu kuipangilia 'Storyline' ili iweze kumuwakilisha zaidi mhusika mkuu katika Project hiyo. Na ukitazama Drama hizo zote mbili zinaelezea maisha ya watawala wawili tofauti katika nyakati tofauti hivyo basi kunakuwa na ulazima wa Project husika kujikita zaidi katika maisha yao mpaka mwisho.
 
Mishil alitumia Sayansi kuwahadaa wananchi ambao kwao Sayansi ilikuwa ni miujiza ya kutetemekewa.

Ndiyo maana Deokman alipotaka kui-Publicize Sayansi Mishil alihuzunika na alimsikitikia sana Deokman.
Yes alikuwa anatumia sayansi ila watu walidhani ana nguvu za kiroho, wenyewe wanaita 'heaven will'
 
Episode za mwanzo ni kama reception, pale ndio mahala pa kukufanya upate hamu ya kuendelea na Drama, nikitumia uzoefu wangu Historical Drama, Maranyingi sana huwa mtindo wa kuanzia mwisho kurudi mwanzo ili uende mwisho( Nadhani hii ndo waswahili mwaita MSAGO), huu mtundo huumpa kiu mtazamaji kuona kipi kilichotokea. Zile Drama zinazoenda moja kwa moja zinahitaji nguvu kubwa ya akili ya mtayarishaji ili akushawishi ili msafiri wote ki- Fikra mpaka mwisho.
 
Naam... shukrani!!
 
Unafahamu zile stori inaendelea halafu inavushwa Kwa Kuandikwa " Mika kadhaa Baade"Three years later"
Pia kuna vituko humo! Siunajua tena Bidam kichwa kibovu!!. Utacheka.
Haha jamaa anajua Sana aisee,kichwa kibovu kile,nimemcheki kwenye series ka 4 ,zote hakuna aliyoharibu,kuanzia bad guy,akijiita shin gun wook
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…