Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Amen. Nimeitamani stock yako. Ngoja na mie nijipange nijaze ila usingizi adui mkubwa wa mission nzima.
 
Kuna mtu anaiangalia hii??ni nzuri??
Nataka kuicheck ila kama nasita hivi
sikubahatika kuiangalia japokuwa niliwahi kuipakua mpaka episode 6,
kule forumsoompi thread ya hiyo drama haina wachangiaji wengi ukilinganisha na drama iliopita (the world of the married couple)

jaribu kuiangalia (wanadamu hatufanani)
 
Baada ya kipindi kirefu kupita bila kudondosha chozi kwenye drama hatimaye nimepatikana mwaka huu, hii drama imejua kuniliza jamani!
IT’S OKAY TO NOT BE OKAY!

Nampenda na kumkubali sana Soo Hyun ila katika drama hii amefunikwa na huyu mwamba aliyeigiza uhusika wa Sang Tae! Mtu anawezaje kuigiza namna ile kama mtu mwenye autism?

Well, my favorite scenes zilikuwa siku ambayo Gang Tae alilala na kutabasamu usingizi, Sang Tae alifurahi sana hadi kesho yake akamnunulia lunch na kumpa pocket money, daaaamn nililia mpaka basi!

Nyingine ni siku waliyoenda kupiga picha ya familia, mwanzoni Gang Tae alikaa ila baadae akaenda, sasa wakati anaingia pale photo studio ile expression ya Sang Tae nako michozi ikanimwagika!

Sehemu nyingine ni pale Sang Tae alipokuwa anamlisha Ko Moon Young halafu Moon Young akawa anamuomba msamaha huku akilia!
Mwisho ni mwishoni kabisa wakati Sang Tae anawaaga kwamba amepata deal la illustration...

Hey, ambao hamjaangalia mtanisamehe kwa kuwaspoil, sikuwa na namna!
 
Hey, ambao hamjaangalia mtanisamehe kwa kuwaspoil, sikuwa na namna!
utakapoamka (niliona tabu kukutafuta kwa waziri mkuu kitambo sana, afadhali umejitokeza)
  1. fanya miujiza yako ile account yangu ife bila ya kupotea data zenu (nimepoteza ile laini mwezi uliopita, taratibu za kuirudisha zimenishinda kwa sababu nina kesi 50 kituo cha polisi)
  2. kuna account nimetengeneza
username: goodwill
=========================

usiku mwema wenye baraka
 
Ile family drama ya tailor nikumbushe jina lote,jana sikuidaka vizuri kule incheon
dah sorry,
hii comment yako ndio nimeisoma leo kwa utulivu.
inaitwa the gentleman wolgyesu tailor shop
==========
lee dong gun
na jo yoon hee mahusiano ya kimapenzi yalianzia hapa, kwa sasa ni wanandoa na tayari waebarikiwa mtoto.
nimeiangalia mpaka episode 5,kwangu naiona ipo vizuri (bila ya shaka una uzoefu mkubwa sana wa kuangalia family drama)
stori zao zinakwenda mwendo uleee wa sikutaki nataka.

humo ndani muna couple ya mwanamama ra mi ran (anatumia jina la Bok Sun-Nyeo kichwa kibovu, kichwa wivu, kichwa fixed, full vituko) na mume wake cha in pyo (anatumia jina la bae sam do).
mke kama yule nampa talaka 50, nyumba namuachia, nguo zangu namuachia (I hope huko mbeleni wataelewana)


 
Hahaha umenifurahisha hapo kwa talaka 50

Kabla sijajibu nimeenda kuwaangalia google kwanza hao wanandoa maana ndoa za mastaa wa kikorea tabu tupu. Wao kwa wao hawawezi dumisha ndoa labda mmoja awe fani tofauti kabisa na ustaa,ndo inaweza kudumu

Basi google ikanipa majibu haya Lee Dong Gun + Jo Yoon Hee Announce Divorce After 3 Years Of Marriage
Then bibie kapata custody ya binti yao mdogo


Ntaiangalia hii nipate uhondo zaidi
 

Usione taabu, karibu wakati wowote...
Pole, kumbe ndio maana nimeona kimya muda sasa.
Nimeshaifuta ile na kuadd hii ya sasa, karibu uendelee kushusha vitu
Shukrani [emoji4][emoji1488]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…