Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Nitaitafuta hio

Maisha ya saiv wengi wanapenda kuishi kwa maigizo
 
Naombeni majina ya series nzuri na za kusisimua za kikorea za kifalme mithili ya JUMONG,six flying dragons,empress Ki,crowned clown,Dong Yi, emperor of the sea(naitafuta) n.k
 
Naombeni majina ya series nzuri na za kusisimua za kikorea za kifalme mithili ya JUMONG,six flying dragons,empress Ki,crowned clown,Dong Yi, emperor of the sea(naitafuta) n.k
Yaani kwakweli hizi season ni kali nataka niirudie Six flying dragon, nikitoka hapo nahamia kwa nchina season inayo itwa Nirvana in fire maana hakuna kama season hizo tena kwa sasa.
 
Ebu niweke kambi hapa.
SteveMollel zicheki hizi utafurahi kwa roho yako "Innocent defendant" kwangu hii ndio best drama of all time nyingine zakuzicheki ni Penthouse, The last, The mask woman na kiporini The empress ki zote hizo zimefutia Sana story zake zimeshiba haswa kuna wakati unaona bando lako linathamani ndogo kuliko ukubwa wa hizo drama.
 
ongezea na hii web series inayoitwa EXO next door.
episode zake ni wastani wa robo saa
binafsi sijabahatika kuiangalia(no comment)
hawa member waliotumika ni wa EXO kweli, yupo baek hyun, exo chanyeol, exo d.o, kai mzee wa dance, suho
===================
Ji Yeon Hee is a 23 year old girl, who hasn't yet dated because she blushes terribly and is completely paralysed when she's near a good looking boy. One day, four members of EXO are trying to keep a low profile, and move into the house of one of the member's grandfather.
However, it turns out that EXO members' house is right in front of Yeon Hee's house.


 
Nilishaiona ila aah kwa upande wangu utoto mwingi
 
move to heaven drama
imetengenezwa na netflix
ina episode 10
aliyekuwa hajabahatika kuiangalia akiwa na muda aitafute, imetoka mwezi huu
nimekuwa mvivu wa kuandika, ingelikuwa kama nyakati zile basi ningeliwapa hadithi nzuri sana na summary
================

Geu Roo ni kijana mdogo anayeishi na tatizo la Aspenger Syndrome, mwanzoni alikuwa akiishi pamoja na baba yake wa kulea (geu roo aliokotwa akiwa mchanga) na walishirikiana kwa kiasi kikubwa sana kufanya kazi ya kukusanya vitu vilivyoachwa na marehemu(kwa mfano mtu amekufa, wao wanahusika na kusafisha vitu vilivyoachwa na marehemu, visivyo na umuhimu vinatupwa na vyengine hufikishiwa wahusika wengine either familia, marafiki au labda mchumba kama marehemu ameacha barua au zawadi yoyote, kazi kumpata huyo mlengwa usiyemjua, hapo ndio utakiona kipaji cha bwana geuroo kwenye uchakataji wa taarifa).

baba yake anafariki hatimaye geu roo anabaki peke yake, lakini kabla ya kupatwa na umauti baba yake alimuachia dhamana ya kumsimamia geu roo mdogo wake aliyekuwa kifungoni.

mjomba wa geu roo ni mpiganaji wa ngumi za kihuni(underground).
je kipi kitatokezea kati ya wawili hao
je wataweza kuwasiliana, kusikilizana na kufanya kazi kwa pamoja?
itafute, kama hujazoea kumenya vitunguu maji jifundishe
=================

kuna uhusiano wowote wa kuwa na tatizo hili la autism na uwezo wa kutatua changamoto ngumu, kipawa maalum (ugenius fulani), au ndio ulimwengu wa drama unatufunza na kutukumbusha juu ya umuhimu wa kuzipa nafasi jamii zote za binadamu bila ya kujali disabilities walizonazo?.
rejea hizi project
  1. move to heaven
  2. its okay not to be okay = licha ya kunyimwa uwezo wa kuwasiliana yule kaka mkubwa alikuwa ni fundi sana wa uchoraji
  3. good doctor = licha ya kunyimwa uwezo wa kuwasiliana bwana yule alikuwa ni genius eneo la afya ya mtoto
  4. marathon movie = muheshimiwa (cho seung woo) alikuwa na tatizo la autism lakini alijaaliwa kipaji cha kukimbia kuliko chui.


 
Wananiacha hoi pale kwenye kukoholea chakula kaambiwa kitu kidogo tu eti anapaliwa na kutemea msosi wootee mezani. bado ule wali wanachanganya kwenye bakuli kuuubwaaa wanashea wengi tena kwa fujo wakorea bana
wakorea wenyewe ni watoto
huoni majibizano yao
mapenzi yao, mara binti kabebwa mgongoni(piggyback riding)
mara mtoto kaiba makeup ya mama yake
 
Hivi mnaposema watu wanataka kuishi maisha ya kwenye tamthiliya mnazungumzia hizi hizi ambazo na mimi naangalia au...? Maana mimi kwa kadri ninavyofahamu drama nyingi nilizoangalia lead actress huwa na maisha ya kawaida au ya chini kabisa..hhata kwa wafilipino nimeona ni hivyo hivyo. In my opinion, kama wadada wakisema waishi kufuata mifano ya kwenye drama basi tutakuwa na wanawake wazuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…