Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Weekend ilisindikizwa na imitation


Ila mmh sijui kiranga gani kilinipata nikaionja hospital playlist kushtuka nipo episode ya 10 kukurupuka hadi wa leo hakuna episode ya 11 halafu ya kumi imeishia patamu. Ongoing ni majanga

List zangu

Imitation(episode 12)genre music,romance,comedy

Rich family's son (episode 100)family drama

Nevertheless(sijaianza)

Modern farmer(episode 20)

Love from today(episode 100 na kitu)

Queen in hyun's man

The spies who loved me(boring ila naenda nayo hivyo hivyo)

family drama navuta kidogo kidogo bahati nzuri zina episode chache hata kwenye server ya FE unapata saiz ya 360
 
nimeshaimaliza kuitazama hii drama, fanya basi kunitumia mtaji wa millioni 100 ili nianzishe biashara yangu na nakuahidi utapata gawio la 20% itakayotokanwa na faida itakayozalishwa, ila usisahau hii biashara niliyoilenga muhasibu nitakuwa mwenyewe (P&L statement itakuwa ni lose kwa miaka 10 kama zilivyo kampuni za uchimbaji madini)
=====================

kizazi cha dhahabu cha wakorea kupitia tasnia ya uigizaji kinachukuliwa na upepo wa umri na hakitoweza kurudishwa tena, ukiwangaalia hawa wazee waliozaliwa kuanzia mwaka 1930 hadi walioshia kuzaliwa mwaka 1969 wanakupa burudani kubwa sana ya kiuigizaji iliojaa tafakari ndani yake yenye kuambatana na mzigo wa maswali yasiojibika.

hiki ninachokishuhudia kwenye televisheni yangu kina uhusiano wowote na maigizo au ni kinyume chake?

kuna hii generation ilioanzia mwaka 1970 nayo inajitahidi sana na bila ya shaka wataziba nafasi za wazazi wao pindi watakapopata pumziko la milele ila nikiwaangalia hawa mabishoo wa siku hizi wanaopakwa lipstick wananipa wasiwasi sana kama wataweza kufikia level ya ubora wa hicho kizazi, wengi wao hubebwa zaidi na umaarufu wao uliochangizwa zaidi na muonekano wao.

Mungu ajaalie pindi hii sanaa ya wakorea itakapomilikiwa moja kwa moja na utamaduni wa kimagharibi niwe nimeshatundiga daluga kufuatilia sanaa yao.
AMEN
 
dae una vituko. Mie nimeganda kwa airtel walipo nipo nao kwa night bundle hope hawatabadili watatutesa sana
namiliki line za mitandao yote maarufu nchini, hao Airtel ninavyowatamani majira ya usiku lakini ndio hivyo network inakuwa spidi ya kobe.
ukipata ubuyu wa unafuu wa MB usisite kunishitua
Halotel mungu anawaona kwa walichotufanyia
 
New Drama Lost Ina Mahadhi Ya My Mister (Najua We Nishabiki Namba Moja Wa Hii) Unaeza Angalia Na hii Pia Japo Iko Nzito Na Emotional.
 
Jung Ho Keun mwamba namkubali sana.
 
New Drama Lost Ina Mahadhi Ya My Mister (Najua We Nishabiki Namba Moja Wa Hii) Unaeza Angalia Na hii Pia Japo Iko Nzito Na Emotional.
ahsante sana,
hizi nyenginezo nazo umebahatika kuziangalia ukanipa fikra (mtazamo) zako juu ya ulichokishuhudia.
  1. hometown cha cha cha
  2. police university
  3. high class
 
Nimemaliza Penthouse nimeipenda sana

nataka niangalie Cruel Palace je ni nzuri?
kiupande wangu sina majibu, niliangalia episode 5 tu takribani miaka 4 iliopita.
kikubwa nilichokiona labda niseme ni harakati za mwanamke zilizochochewa na kisasi, zinazomzalishia ndoto ya tamaa za kuumiliki mfumo dume kwenye ulingo wa siasa kwa kumtumia mwanawe baada ya kuonjeshwa ladha ya maisha ya familia ya kifalme.

labda nimwite huyu mkorea wa kizimkazi anayeitwa Great Conqueror anaweza kukupa tathmini yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…