Kwa wapenzi wa Korean Dramas, hii ni thread yako!

Mwaliko Basi Chingu Nije Kula Biriani.

Amia tu, Fanya Kitu Roho Inafurahia.
watoaji mualiko wa harusi ni wanawake, unakwenda harusini huna hata sare hapo lazima vishakunaku wakuseme pembeni.
huyu mmasai mwenye kiuno cha mdudu ubuyu ametokea wapi?
kuepusha hilo ngoja nikufanyia maombi ya mualiko
============
ngoja nijiandae vya kutosha baadae nitafanya hivyo
 
Mie niligekuwa mpenzi, wa series na single movies za Asia sababu ya kuvutiwa na tamaduni zao, lakini pia series zao nyingi upoamua kuwa mtazamaji makini unapata Darasa. Ukweli ni kwamba Hicho kizazi cha hao wazee walikuwa wanaishi sanaa kwa misingi ya Tamaduni zao,lakini uvaaji wa uhusika. Binafsi sijaona hawa watoto 1990s ambaye ana hata theluthi ya kipaji kama cha hao wazee, kama ulivyosema wengi kazi kujipodoa. Angalau kizazi cha kina Choi seo jeon( wang gun), Jang hyuk( Dae gil), Song ill gook( Jumong), Lee byung hun( IRIS). Kidogo kizazi cha hawa wapo vizuri sana. Lakini hawa mabishoo zako Seoul kazi wanja tu. Ndio maana maranyingi naanglia series kwa kurudi miaka ya nyuma maana wazee wanamadini kwenye sana.
Series kama Hwarang, huwezi ukaiweka hata meza moja na dude kama Emperor of sea, Damo n.k kifupi vijana wanachosha kuwatazama lakini hao wazee ni habari nyingine.
( Note): Mie sivutiwi na tamaduni za kimagharibi.

Duh! Mara hii ushaimaliza Sang do!!! Hur jun je?!
 
On the verge of insanity - hii ep ya 11 nimekua eti
Niko na hometown cha cha cha
Hospital playlist
The road: tragedy of one
Misty
Bossam nimeishia ep 14 kama matukio ni marudio hivi

@Damushin nimemaliza kumtazama ha hyun woo kwenye mask singer doh sio poa Yule binaadam

Naamin walimchoka au nae alichoka, Yule alomtoa hakuwa mkali kiivo kuzid Yule dada( nshawasahau)
 
Gyeoul kuja hapa Mara moja,
Huyu Emma Raducanu ana ubora gani?
tokea Jana nawaona wapenda kelele wa ulimwengu huu(waengereza) wamekuwa wakimsifia sana huyu binti, hivi ana potential ya kuwa na ubora kama waliokuwa nao malegendary wa kike mfano Serena Williams na Venus, Dada maria sharapova n.k

Kwako mtaalamu wa huu mchezo wa tennis
 
She is Good, Very Good Kwa Umri Alonao Sasa Na Nafasi Aliyofikia Yupo Vizuri,

Waingereza Si Unajua Hawanaga Dogo Vyakwao Wanajua Kuvithamini.

Ila Uzuri Ni Kwamba Bado Ni Mdogo Na Ananafasi Ya Kufikia Level Izo, Sijawai Kuwaona Wakina Serena Kwa Umri Kama Huu Kwaiyo Sitokua Na Majibu Straight.

Na Chengine Imekua Ni Kubwa Sana Ni Namna Alivyoweza Kufika Final Na Kuchukua Uchampion, Alicheza Qualifying Match Kama 3 Ili Kuingia Kwenye Main Draw Then Ameenda Kwa Straight Set Mpka Uchampion Na Yupo Ranking 150 Uko Yaani Yupo Nje Ya Zile Top 100.

Kufikia Kiwango Cha Kina Serena Nampa Iyo Nafasi Kwa Namna Ya AnavoServe Alivyo Mtulivu Na Mental Yupo Vizuri
Maana Tennis Kama Ubongo Uko Kulia Na Wewe Kushoto Unatolewa Mapema Tu.
 
Na Uzuri Niliona Tu Akishinda Jana Ningejua Ningebet.

Nasubiri Final Ya Leo Maana Naiona 5Set Na Natamni Sana Medved (Favorite) Ashinde Leo Maana Anastahili Japo Djovik Nae Mmmmh!
 
Nipo Ep ya 10 nimeipenda.

Samahani unaweza nisaidia kunitajia nyingine ya Historical ya mapanga mapanga
hizi historical drama au wenyewe wanaziita sageuk kwa lugha ya kwao zimegawanyika (zipo fusion, nyengine zimetokana na forktale, traditional, epic sageuk n.k). Na pia zimegawanyika kwa mujibu wa kipindi husika cha muda na kila muda zilishuhudiwa tawala tofauti za kiutawala ambazo zimerekodiwa na waandishi wa kihistoria

kwa ufupi hizo za mapanga unazozizungumzia wewe tumeshuhudia vituo hivi vya televisheni wakituzawadia zaidi drama zinazohusu tawala za:
  1. Goguryeo(koguryeo)
  2. Baekje
  3. Shilla dynasty
  4. Goryeo (koryeo)
  5. Joseon
  • kunzia namba 1 hadi 3 zinaitwa three kingdoms
  • kuanzia namba 3 hadi 4 zinaitwa later three kingdoms (sijakosea, utanielewa mbele)

Tuanze na Goguryeo, baadhi ya drama zake ni hizi (nimekuwekea kwa mtiririko wa historia):
  1. Jumong (prince of the legend): utajifunza maisha ya huyo chumong kuanzia kuzaliwa kwake mpaka kufikia hatua ya kuanzisha taifa la Goguryeo.
  2. the kingdom of the winds (the land of the wind): hii inaelezea maisha ya mfalme yuri (mtoto wa jumong) na maisha ya mwanawe aliyeitwa muhyul (baadae aliitwa Daemusin).
  3. princess jamyung: stori ya princess wa nakrang of nangnang kingdom aliyependana na prince hodong wa Goguryeo, Hodong ni mtoto wa huyo Muhyul
  4. Gwanggaeto, The Great Conqueror: itakupa simulizi ya maisha ya shetani mtu anayeitwa Damdeok aliyetawazwa mfalme wa 19 wa Goguryeo baada ya kifo cha baba yake, na kwa nini aliitwa the great conqueror
  5. the legend: hii nayo pia inazungumzia maisha ya damdeok
  6. river where the moon rises: stori inayomuhusu princess pyeonggang na mumewe on dal.
  7. yeon gae somun: hii inazungumzia maisha ya huyo bwana mkubwa.
  8. dae jo yeong: maisha ya huyo bwana dae aliyeanzisha taifa la balhae baada ya kuangushwa kwa taifa la goguryeo, ilimchukua takribani miaka 30 kuitimiza hiyo ndoto.

Drama zinazozungumzia utawala wa Baekje
  1. king geunchogo (the king of legend): inazungumzia maisha ya huyo chogo aliyekuwa mfalme wa 13, alifanya mazuri yake hususani kwenye uwanja wa vita na kuipaisha baekje dhidi ya maadui zao na ndugu zao wa damu wa goguryeo
  2. ballad of seodong; love story kati ya mvulana wa baekje na princess wa shilla(matifa mwili maadui)
  3. gye baek: maisha ya general gye baek aliyekuwa nguzo ya mwisho ya utawala wa Baekje

Drama zinazozungumzia utawala wa Shilla
  1. kings dream ( dream of the empire): utajifunza maisha ya watu mashuhuri wa shilla kama vile kim chunchu, queen seondeok, queen jindeok, kim yushin. hii inaelezea jinsi shilla ilivyoweza kuyahodhi mataifa mengineo mawili ya koguryeo na baekje na hatimaye kuwa emperor.
  2. emperor of the sea (haeshin): maisha ya jang bogo
  3. hwarang: boys over flowers wa kipindi hicho nchini shilla
hizo ndio drama za three kingdoms
Drama zinazohusu utawala wa Goryeo na joseon zitakuja siku nyengine (nakhofia hapo kwa joseon nitaandika mpaka kesho)
===========================

unywaji pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako ila ni faida kwa TRA
 
Hahahaa eti boys over flowers. .una nini lakini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…