Finegirlone
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,836
- 3,609
Habari zenu wapendwa, amani iwe nanyi
Kwa kuanza bandika sufuria lako la maji jikoni ila maji yanatakiwa yawe mengimengi kuzidi kiasi cha mchele tofauti na ule wali wa kukadilia maji kutokana na kiasi cha mchele.
Baada ya maji yako kupata moto tia chumvi kulingana na kiasi unachopenda, funika acha ya chemke.
Baada ya kuchemka tia mchele wako ulioshwa na kulowekwa kama dakika kadhaa hata kama haujaloweka sio kesi ila mchele ukitaka unyooke uwe mtamu ni vema kuloweka dakika kadhaa hata saa kabla ya kuupika.
Uchemke hadi ufikie kiasi cha kuwa mgumu hivi ukiutafuta kama unaugumu fulani lakini ile hali ya ubichi wa mchele ushapotea umebaki mgumu.
Epua, chukua chujio lako kubwa na bakuli kubwa au sufulia ama vipi utafanya kusudi ni kuuchuja ule mchele, yale maji mwaga halafu mchele urudishie kwenye sufuria yako ileile rudisha jikoni, tia mafuta kwa juu ya wali kiasi upendacho hata kama haupendi mafuta sio lazima kuweka, seti moto wako hafifu kiasi, kama jiko la mkaa pia fanya moto mdogo sana maana wali umebaki hatua ndogo kuiva kwa hiyo hauhitaji moto mwingi, baada ya dakika 5- 7 utakuwa umeiva.
Tayari kwa kuliwa, kwa njia kamwe hautopika bokoboko au kuunguza chakula.
Sent using Jamii Forums mobile app