Kwa wataalam na wazoefu wa pikipiki

Kwa wataalam na wazoefu wa pikipiki

covid 19

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2014
Posts
6,967
Reaction score
17,452
Kwa Wataalamu wa Pikipiki:

Ninatafuta ushauri kuhusu aina au brand bora ya pikipiki kwa kazi za kubeba mizigo kati ya kg 30 hadi 75 kila siku.

Je, ni brand gani kati ya boxer, tvs, hero, honda, hunter na nyingine. Je ipi ni imara na inadumu muda mrefu kwa mazingira ya joto, vumbi, na mvua ya Dar es Salaam?

Ninalenga pikipiki ambayo itahimili kazi ya kila siku bila kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara.

Nipe uzoefu wako ili kusaidia kufanya maamuzi sahihi!
 
Nasubiri ushauri wenu wakuu
 
Kuna tofauti kubwa kati ya Luxurious pikipiki na Ordinary pikipiki.

Luxurious pikipiki (mfano boxer)
-Ni comfortable kwa abiria
-Zinapendwa maeneo ya mjini
-Zinatumia mafuta kidogo zaidi
-Zinataka barabara za lami zaidi
-Zina speed kubwa
-Gharama yake ya manunuzi ipo juu kidogo (more thans 15%)
-Zinahitaji services ya uhakika na vipuri vyake viko juu zaidi.
-Ni pikipiki ya ubishoo fulani
*Ukiachana na kufaa kwa matumizi binafsi, kibiashara inataka utumike mjini zaidi (kwenye lami), kubeba abiria (labda na mizigo midogo midogo), na mwisho hiyo kazi uwe unaifanya mwenyewe zaidi kuliko kumpa mtu.

Ordinary pikipiki (mfano Kinglion)
-Inafaa popote (mijini, porini, milimani), kubeba mizigo na abiria
-Sio comfortable kuendesha au kubebwa abiria.
-Bei ni nafuu kidogo kuinunua na kuifanyia service
-Ni imara na vumilivu
-Haina mvuto sana kwa abiria wa mijini (Dar!).

Kwa ushauri wangu, kama unataka pikipiki ya biashara ya abiria au matumizi binafsi maeneo ya mijini, Boxer itakuwani chaguo bora. Na kana unataka pikipiki ya kazi kazi, mazingira yoyote yale, Kinglion ni chaguo sahihi zaidi.

Sasa kupanga ni kuchagua.
 
Boxer au tvs itakufaa nimeendesha pikipiki za kichina na nimeendesha pikipiki za india
 
Back
Top Bottom