Kwa Watakaohitaji Viwanja

Sabi Sanda

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
409
Reaction score
31
Salaam

Kwa wale ambao (au ndugu zao au rafiki) watahitaji kupata viwanja vilivyopimwa maeneo ya Kerege naomba tuwasiliane. Kwa sasa nimeanza utaratibu wa kubadilisha matumizi ya shamba langu la ekari 36.8 kuwa eneo maalumu la makazi ya watu. Eneo hili liko mkono wa kulia kama unatokea Dar kwenda Bagamoyo na ni umbali wa km 1.5 toka barabara kuu iendayo Bagamoyo. Kerege iko umbali wa km 23 toka Tegeta au km 10 toka Bunju ukielekea Bagamoyo. Viwanja vitakuwa na ukubwa wa angalau mita za mraba 900 kwa kila kiwanja na bei ya mita moja ya mraba itakuwa ni shilingi 8,500. Taratibu zote zinategemewa kukamilika kabla ya mwisho wa mwezi Juni mwaka huu. Ndani ya Kijiji cha Kerege Kamal Group wanajenga the largest Industrial complex in Tanzania. Kwa anayehitaji (mtu binafsi, kikundi, Saccos, kampuni au taasisi) tuwasiliane kwa simu namba 0659 281964.
 
Mh Mimi nilitaka kuchangamkia lakini hilo jina SANDA pamoja na ukweli kuwa eneo hilo linatakiwa kuwa Industrial area imenitisha kidogo! Twende Taratibu Jamani
 
hiyo bei mbona kubwa ajabu (8500*900=7,650,000). Na ni ikerege kisa jamaa wamejenga kiwanda karibu. Mi simo wajaribu wengine
 
Ni vizuri kuwa na kiwanja lakini kama kuna mpango wa kuanzishwa kiwanda sidhani kama kutafaa makazi ya watu
labda kwa ajili ya biashara
 
Waliohamia karibu na hayo maeneo wanavamia kila siku wanaibiwa na wake zao kubakwa!.Wewe unatuhakikishiaje usalama wetu?
Pia hu umeme wa mgao sizani kama kuna any investor these 4 years atakuja kuwekeza kwenye hiyo EPZ ya karibu na hizi sites!.Wazungu(wawekezaji)wanasikiliza sana kauli za wausika popote pale(MOM wa Umeme)Ngereja asatamka oficial kuwa mgao wa umeme utatokomea ifikapo 2014 kama sikosei!.So no banker nor any investor will come to invest before 2014.kwani apa tuna CNN,BBC,Aljeseera.So tupe huakika Ndugu
 
hiyo bei tu! kiwanja kimoja + gharama za usafiri kila siku kwa mwezi tu nanunua nyumba mbagala hata kama nyumba mbele jalala
 
Naomba kujua kama bei inaweza kupungua na mfumo wa malipo (say two installments)
 
Naomba kujua kama bei inaweza kupungua na mfumo wa malipo (say two installments)

Uwezekano wa kupunguza bei kiasi upo na pia itawezekana kulipa kwa awamu. Ni suala la kukubaliana.

Naomba niwatoe wasiwasi hali ya usalama ni nzuri. katika mpango huu tutahakikisha kuwa na maji pia yanapatikana eneo la viwanja.

Wakuu, hiyo bei ni ya kawaida kabisa. Ukienda Bunju B kiwanja kilichopimwa huwezi kupata chini ya shilingi milioni 15 na vinapanda bei kila uchao.
 
Ni vizuri kuwa na kiwanja lakini kama kuna mpango wa kuanzishwa kiwanda sidhani kama kutafaa makazi ya watu
labda kwa ajili ya biashara

Viwanda viko mbali kabisa na eneo hilo. viwanda viko mkono wa kushoto wa barabara iendayo Bagamoyo.
 

je? Bei hiyo ni pamoja na gharama ya hati ya umilikishwaji wa kiwanja?
 
je? Bei hiyo ni pamoja na gharama ya hati ya umilikishwaji wa kiwanja?

Kama tukiwasiliana mapema na ukaweza kulipia kabla ya kupeleka majina ya wamiliki kwa kila kiwanja then hutahitajika kulipia gharama za hati.
 
Ni heri umezungumza mapema mpaka kufikia june majibu yatakuwa tayari kichwani mwangu, maana hili suala inabidi kulifanyia kazi kidogo. Maana hapo unazungumzia karibu Kilomita miamoja kutoka expected home mpaka Posta na kurudi.
 
Ni heri umezungumza mapema mpaka kufikia june majibu yatakuwa tayari kichwani mwangu, maana hili suala inabidi kulifanyia kazi kidogo. Maana hapo unazungumzia karibu Kilomita miamoja kutoka expected home mpaka Posta na kurudi.

Unakaribishwa sana.
 

Hivi na wewe unajiita great thinker ?
 
Inaonekana kwa hiyo bei ilivyo kubwa na wewe unataka upate ya kujenga kiwanda
Pungusaaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…