Kwa watia nia, nimejifunza yafuatayo

Kwa watia nia, nimejifunza yafuatayo

mheshimiwamtemi

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2014
Posts
291
Reaction score
218
  1. Ubunge kwa uchaguzi huu ni hisia sio uwakilishi
  2. Watia nia ni wengi kuliko chaguzi zilizopita
  3. Vijana ndio wanaongoza kutia nia japo wengi wao hawajulikani jimboni maana wanaishi mijini tuu
  4. Wasanii nao wameona mifano ya watangulizi wao hivyo hawako nyuma
  5. Wabunge vigogo au waliokuwa mawaziri wamegawana majimbo bila kuingiliana hii ni dhahiri vijana wengi watakosa
  6. Ubunge una pesa nyingi na thamani ya juu kuliko teuzi za Rais
  7. Siasa na dini havitengani maana viongozi wa dini wanahubiri siasa
  8. Vyama vya siasa vina wateule wao hivyo wengi wa watia nia wanajisumbua tuu au wanaandaa C.V zao
  9. Vyana dhaifu vingi vitakosa wawakilishi Bungeni
  10. Wananchi watakosa wawakilishi makini Bungeni
Asanteni
 
Huu ndio ulikuwa wakati wa sisiemu kukisafisha chama kwenye kura za maoni,ila utaona wapiga dili wakirudi tena mjengoni.
 
Huu ndio ulikuwa wakati wa sisiemu kukisafisha chama kwenye kura za maoni,ila utaona wapiga dili wakirudi tena mjengoni.
Unajua ccm wanajiona wamemudu kuwaaminisha watanzania kuwa wao ni bora ndio maana wanarudi kwenye uhalisia wao
 
Back
Top Bottom