Kwa waungwana pekee

F.c.mwanzi

Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
65
Reaction score
17
Wana JF habari zenu,
Ni mwaka sasa toka nimemaliza shahada yangu na sijafanikiwa kupata kazi ya kuajiriwa moja kwa moja, binafsi ninaona muda si rafiki kwangu kutokana na malengo yangu.Hivyo ninaona ni bora niangalie upande wa pili wa shilingi yani kujiajiri.

Ingawa kuna kipindi nilipata kazi za mda mfupi pamoja na internship ktk bank fulani ambapo walinipa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya usafiri na chakula sikufanikiwa kuweka akiba kutokana na mazingira niliyo kuwa nayo. Pia angel finance kwa upande wngu imekua vigumu kupata kama mjuavyo sio watu wote wana bahati ya kupata ndugu/wazazi wenye uwezo kifedha kwamba utamweleza mipango uliyo nao kisha akaku support hasa kifedha.

Hivyo ninaona nianze biashara ndogo ambayo nina uzoefu nayo,kwani niliifanya kipind nikiwa chuo na ilinisaidia kwa matumizi madogo dogo,badaye nitakapo pata mtaji wa kutosha nita nitabadilisha.

Biashara ninayo taka kuanza nahitaji mtaji wa kuanzia sh.laki 5,kwa mtaji huu ktk wiki 3 unaweza kuingiza laki 170-220 kama faida baada ya gharama zote.

Hivyo naomba msaada wa mkopo wa fedha laki 5 kwa yoyote mwenye nayo ila nitamlipa kwa riba ya 20% yaani nitampa laki 150 kila mwezi ndani ya miezi 4,na kukamilisha lak 5 na laki 1 kama riba jumla kuu itakuwa laki 6 nipo tayari kumpa academic certificates zangu awe nazo kama dhamana kwa kufuata makubaliano hadi nitakapo mrudushia fedha yake yote na unaweza kujilidhisha na mahali nilipo yani ninapo ishi pamoja na vitu vingine.wana Jf naomba msaada wenu kwa hili nimechoka kukaa nyumbani na kusubiri miujiza ya kupata kazi ni bora hyo kazi inikute na pambana.maisha yamekuwa magumu sana kwa upande wangu kwa wasamalia mwema,kwa aliye tayari anawe ni PM.

Pia nakaribisha mawazo mbadala yatakayo niwezesha kutoka ktk hatua hii niliyo nayo.
Nawasilisha
 
Pole sana ndugu yangu I hope utapata msaada mzuri hapa jf
 
4 yrs bila kuajiriwa....pole, Naamini wenye cha ziada watakuja hapa, ila digirii yako ilisomea nini?
 
kila la kheri kaka... ila sijui unishirikishe hako kabussiness idea kwenye pm!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…