siyo kweli mkuu ila ni imani potofu tu. labda nikupe sababu ambazo zinaweza kumsababishia mtoto kuumwa na mtu akazi relate na hali ya ujauzito wa mama.
mama anapokuwa mjamzito huwa kwa sababu ya uchovu, na maudhi ya mimba basi hupunguza concetration kwa previous babies. mara nyingi hujikuta anajishughulisha sana na maudhi ya mimba kuliko mtoto na kwa hili huwez kumuhukumu mama hata kidogo. sasa anapokuwa na hali hii mtt hujikuta akitengenezewa mazingira ya kujitetea mwenyewe like anaeza kuachwa acheze kwenye kochi sebulen mida ambayo mbu ni wengi na akawa na furaha tu, lkn hatma yake ni kuugua malaria. istoshe kwenye familia moja malaria ikiingia kwa mmoja basi kwa wengine ni rahisi sana kupayta kwani mbu huwauma kwa kupokezana so mara nyingi sana mama mjamzito hupata malaria na akasababisha wengine humo ndani kupata malaria.
point yangu ya msingi sasa kutokula kwa mtoto ni side effects ya dawa za malaria, lkn pia uangalizi wa jinsi ya kumlisha na aina za vyakula anavyokula mtoto. ushauri hapa mkeo aongeze apenzi kwa mtoto huyu lkn pia ajaribu kumbadilishia mtoto aina za vyakula na hata maeneo ya kumlishia ili mtt asikinai msosi. pia ampe dawa za minyoo pamoja na juice ambazo ziitamwongezea mtoto hamu ya kula.
pole sana na kamwe usimtenge mtoto na mama yake wewe baba waweza kuchukua jukumu la kumkumbatia na hata kumlisha mtoto huyu uwapo nyyumbani.