Kwa wenye bajaji........kati ya Tvs na re 4 205 ipi bora

Job Richard

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
3,876
Reaction score
2,190
Nimejitahidi kupata maelekezo ya hizi aina mbili za bajaji

re 4 205 wanaisifia wengi ni ngumu na imara lakini shida ipo kwenye engine kuchangannyika na oil ni haraka
kuliko Tvs king

na kwa upande wa Tvs wengi wanadai wanauza jina tu na kujipanga kwao ila si lolote kwa barabara zetu za vumbi
ipo kama boxer Bm pikipiki
lakini ndizo nyingi hebu tuelewashane hili wajuvi

hizi Re zipo mbili two stroke na four stroke kama ndizo ngumu mbona chache sokoni na hili la kuchanganya oil vipi?
 
Tvs ni bora kwa uimara pamoja spare za kumwaga, na mafundi ni weng ila re4 nzur kwenye speed tu, na haiuzuki second hand pia spare zake gharama na mafundi wachache ni hayo tu
 
Asante sana mkuu nashukuru na kwenye engine kuchanganya oil nalo ni kweli?
 
Bajaji bora ni RE 4S kwa sababu ni ngumu na inadumu muda mrefu, muhimu ni services na upate dereva mzuri, kuhusu spares zake original ni gharama kidogo pia zipo za bei rahisi kama za SK. TVs ni nzuri ikiwa mpya lakini zinawahi kuchoka pia spare zake original ni ghali sana, kama unabisha nenda posta katika duka lao. Kizuri spare zake za kichina ni nyingi. Kwa ushauri wangu chukua RE 4S hutajuta.
 
duuuh kiukweli unabaki katikati okay lakini mkuu

vipi kuhusu kuchanganya oil na kingine wengi wamekimbilia Tvs kuliko Re 4s na je spare zake za kichina zipo? maana naona hapa ndipo panafanya re 4s wengi waikimbie

maana ushauri niliopewa ni huu
nunua re lakini ujue itakuwa yako forever maana haziuziki na vifaa ghali pia mbovu ni majibu niliyopewa katika kuuliza kwangu
 
Kwa ujuzi wangu kama ambavyo waliyo tangulia walivyo sema, lakin kila mutu anavutia kwake ngoja na mim nitafute upande wangu..... Nimeanza kujihusisha na utengenezaji wa hvi vyombo toka 2009 - 2013 na ninacho kijua nikwamba four stroke ndio bajaji ambayo ikimaliza miez 6-8 inakuwa imechoka na sokon kupata mteja inakuwa ngumu, ila kwa tvs ni nzur na inaweza kudum 8-10 month na sokon bado inauzika sema spea zake ndo kimbembe lakin yote kwa yote ni utunzaji wa dereva tu na ufuatiliaji wa service ambalo Mara nyingi wamiliki hukimbia hapa.... Kama ni mimi ningechagua tvs
 
inachanganya oil na nini??? , mm ni fundi wa RE
 
Nimejitahidi kupata maelekezo ya hizi aina mbili za bajaji

re 4 205 wanaisifia wengi ni ngumu na imara lakini shida ipo kwenye engine kuchangannyika na oil ni haraka
kuliko Tvs king

na kwa upande wa Tvs wengi wanadai wanauza jina tu na kujipanga kwao ila si lolote kwa barabara zetu za vumbi
ipo kama boxer Bm pikipiki
lakini ndizo nyingi hebu tuelewashane hili wajuvi

hizi Re zipo mbili two stroke na four stroke kama ndizo ngumu mbona chache sokoni na hili la kuchanganya oil vipi?
Mkuu, kwa upande wangu ningekushauri uwe na TVS King kwa kuwa ni bora sana ukilinganisha na Bajaji. TVS ina uwezo wa kustahimili kwenye barabara za vumbi ukilinganisha na Bajaji ambazo zenyewe zina perform vizuri zaidi kwenye barabara yenye rami. Pia, TVS una uwezo wa kuiuza kwa bei nzuri tu baada ya kuitumia kwa kipindi cha miaka miwili or so, ila Bajaj ikishaanza kuchoka ujiandae kumaliza nayo.
 
Kwa ujuzi wangu kama ambavyo waliyo tangulia walivyo sema, lakin kila mutu anavutia kwake ngoja na mim nitafute upande wangu..... Nimeanza kujihusisha na utengenezaji wa hvi vyombo toka 2009 - 2013 na ninacho kijua nikwamba four stroke ndio bajaji ambayo ikimaliza miez 6-8 inakuwa imechoka na sokon kupata mteja inakuwa ngumu, ila kwa tvs ni nzur na inaweza kudum 8-10 month na sokon bado inauzika sema spea zake ndo kimbembe lakin yote kwa yote ni utunzaji wa dereva tu na ufuatiliaji wa service ambalo Mara nyingi wamiliki hukimbia hapa.... Kama ni mimi ningechagua tvs
asante sana mkuu nashukuru nami nimeongea na mafundi wengi wamenishauri niachane nayo re 4s wengi wao wamenieleza kwenye kuiuza ndipo shida ilipo bila hivo ukubali ikufie mkononi mwako
 
Mkuu, kwa upande wangu ningekushauri uwe na TVS King kwa kuwa ni bora sana ukilinganisha na Bajaji. TVS ina uwezo wa kustahimili kwenye barabara za vumbi ukilinganisha na Bajaji ambazo zenyewe zina perform vizuri zaidi kwenye barabara yenye rami. Pia, TVS una uwezo wa kuiuza kwa bei nzuri tu baada ya kuitumia kwa kipindi cha miaka miwili or so, ila Bajaj ikishaanza kuchoka ujiandae kumaliza nayo.
asante sana mkuu nashukuru sana
 
inachanganya oil na nini??? , mm ni fundi wa RE
oil na petrol mimi sio fundi sina utaalamu wowote huko bali nilitaka kumiliki je hilo la kuchanganya ni kweli? pia kama fundi wa Re nini ushauri wako mkuu please
 
hakuna kitu kama hicho cha kuchanganya oil na petrol. Nunua RE 4S mpe dereva mzuri zingatia services ndio uchawi wake.
 
Kwa ujuzi wangu kama ambavyo waliyo tangulia walivyo sema, lakin kila mutu anavutia kwake ngoja na mim nitafute upande wangu..... Nimeanza kujihusisha na utengenezaji wa hvi vyombo toka 2009 - 2013 na ninacho kijua nikwamba four stroke ndio bajaji ambayo ikimaliza miez 6-8 inakuwa imechoka na sokon kupata mteja inakuwa ngumu, ila kwa tvs ni nzur na inaweza kudum 8-10 month na sokon bado inauzika sema spea zake ndo kimbembe lakin yote kwa yote ni utunzaji wa dereva tu na ufuatiliaji wa service ambalo Mara nyingi wamiliki hukimbia hapa.... Kama ni mimi ningechagua tvs
Samahani ndugu, wewe kama fundi baja unashauri nini juu ya swala la kununua tvs king kwa mtu kwa lengo la kufanya biashara. Je, inaweza kuludisha gharama au ni bahati nasibu sana(kumbuka sitomkabidhi dereva, nitaendesha mwenyewe)
 
Inalipa tena Kwa mda mfupi kama utaendesha we mwenyew kuliko kumpa Mtu,
 
Iv niandae kam shiling ngapi niwezekupata tvs king ambayo babo inadai(ipo vizuri kwa muonekano adi injini yake) kiufupi iwe haijamaliza ata mwaka1 tokea itoke dukani. Nijipangeje apo kaka.
 
Tvs ni nzuri na hata spaire zake ni raisi kupatikana na garama za spaire ni nafuu kidogo tofauti na nyingine.
 
Kuna kipindi mimi nilitaka kununua bajaji kwa ajili ya biashara.
Nilikwenda dukani na kukuta bei ya TVS ni milion 7, nikaazimia kuinunua moja.
Lkn mtaani nikakutana na mtu akanishauri ninunue used, hoja aliyotoa ni kwamba bajaj hata ununue mpya hesabu yake barabarani haizid elfy 20 kwa siku, na pia ukiitumia mwaka tu thamani yake kwa kuuza inakua milion nne/nne na nusu.
Nikashawishika!
Ninavyoongea hapa nimenunua TVS tatu kwa gharama ya milion kama 12 jumla.
Hesabu ni sh elfu 20 kwa siku na nachukua kwa siku 5 tu kila bajaji, hizo siku nyingine ni pesa ya service. Nimepanga kuziuza zote baada ya mwaka, pesa yangu itarudi na faida kama milion 2 hivi, nikiongeza na pesa ya kuziuza nakua na faida mlima.
Nakushauri ununue TVS kwa sababu kibiashara hata madereva wanazipenda kuliko aina nyingine.
 
Nashukulu kwa mawazo yako ya kujenga, nimepata cha kujifunza kutoka kwako. Siku si nying nitanunua tvs king ya kwangu(used) alafu vipi kuhusu ununuaji wa bajaj kwa mtu hakunaga showroom maalum kwajili ya tvs za mtumba kama tunavyoona showroom za magari?
 
Kama kuna showroom mimi sizijui. Binafsi nilizunguka na fundi kwenye vijiwe vya bajaji, huko kuna bajaji nyingi tu zinauzwa.
Bajaji 2 ambazo nilinunua milion 4+ kwa kila moja zimenyooka sn maana zimetumika mwaka mmoja kila moja, na hiyo nyingine ina mwaka na nusu.
Muhimu uwe na fundi ambae ataikagua kabla ya kuipaitisha kuwa inafaa. Hata hizi zangu zilihitaji service licha ya kuzikuta barabarani, lkn si service kubwa.
 
Back
Top Bottom